Jumapili, 7 Julai 2024

VIONGOZI MBALIMBALI WA MAHAKAMA NA SERIKALI WATEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA SABASABA

Viongozi mbalimbali wa Mahakama na Serikali pamoja wametembelea Banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), 2024 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Temeke Dar es Salaam.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio ya Viongozi waliotembelea banda la Mahakama;




Picha za juu ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina (mwenye suti ya 'dark' bluu) akiwa katika mabanda mbalimbali yaliyomo ndani ya banda la Mahakama ya Tanzania alipotembelea banda hilo jana tarehe 06 Julai, 2024 katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), 2024 yanayoendelea.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura akisaini kitabu cha wageni ndani ya Mahakama Inayotembea. IGP Wambura alitembelea banda la Mahakama ya Tanzania jana tarehe 06 Julai, 2024 katika Maonesho ya (Sabasaba) yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Temeke jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura akiwa katika mabanda mbalimbali ya Mahakama na Wadau alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania jana tarehe 06 Julai, 2024 katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Temeke jijini Dar es Salaam.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo cha Usuluhishi, Mhe. Zahra Maruma ( mwenye nyuo yenye rangi nyeusi na nyeupe) akiwa katika mabanda alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania lililopo kwenye Maonesho ya (Sabasaba).
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo cha Usuluhishi, Mhe. Isaya Arufani (aliyeketi) akiwa ndani ya banda la Mahakama alipotembelea maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), 2024.
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, mhe. Chiganga Tengwa (mwenye fulana nyekundu) akiwa kwenye baadhi ya mabanda katika maonesho ya (Sabasaba) yanayoendelea.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni