Jumapili, 7 Julai 2024

UJENZI WA MAHAKAMA YA MWANZO HAUBI KICHOCHEO CHA MAENDELEO

Na. TAWANI SALUM-Mahakama, Kondoa

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel tarehe 2 Julai, 2024 alikabidhi kwa Mkandalsi Molad eneo itakapojengwa Mahakama ya Mwanzo Haubi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Ole Gabriel aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya miradi kama hiyo.

“Napenda kusema kwamba na ielewke kwa wananchi kuwa Mahakama haifanyi biashara ambacho mnaweza kuishukuru Mahakama ni kufanya utaratibu na mchakato wa kuhakikisha kwamba inajenga hoja Serikali ikaelewa na kutenga fedha,” alisema.

Mtendaji Mkuu alieleza kitu cha pili ambacho Mahakama inafanya ni kuamua Mahakama inajengwa wapi mara fedha ikishapatikana.

Kadhalika, Prof. Ole Gabrierl aliishukuru Wizara ya Sheria na Katiba inayoongozwa na Mhe. Balozi Pindi Chana pamoja na Msaidizi wake Naibu Waziri, Mhe. Jumanne Sagini ambao ndio wanashughulika na masuala ya sera, kusoma bajeti ya Mahakama bungeni na hatimaye  kupatikana kwa fedha.

‘’Niwashukuru sana wataalamu wetu ambao wamefanya kazi hii pamoja na timu yangu yote, wameshirikiana na Mtendaji wa kanda. Mimi nimekuja tu kumalizia, ila wao ndio walioifanya kazi hii,” alisema.


Mshauri Elekezi, Bw. Robert Modu akikabidhiana nyaraka Mkuu wa Kampuni ya Moladi, Bw. Kim Mgaya. Nyuma ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa na wadau mbalimbali katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Haubi, Wilaya ya Kondoa.


 
Sehemu ya watumishi, wananchi na wajumbe walioudhuria makabidhiano ya mradi wa Haubi Wilaya ya Kondoa wakisikiliza kwa makini maelezo anayotoa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa makabidhiano hayo.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyeshika jembe) akiweka alama katika kiwanja ambacho Mahakama ya Mwanzo Haubi itajengwa. Nyuma ni Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manoti.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Mahakama pamoja na akina mama wa Kijiji cha Haubi wakijadili jambo kwa pamoja.

Kushoto ni Bw. Kim Mgaya, ambaye ni Mkuu wa Kampuni ya Moladi akiwa na wadau wengine wakijadili jambo wakati wa makabidhiano hayo.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa na Msanifu wa Majengo, Bw. Revocatus Bigambo wakijadili jambo pamoja na wadau wengine.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa na Mkuu wa Kampuni ya Moladi, Bw. Kim Mgaya na Bw. Robert Modu (kushoto) wakiwa na nyaraka za ujenzi ikiashiria kuanza kwa ujenzi huo.

Kushoto ni Revocatus Bigambo ambaye ni Msanifu wa Majengo akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel mipaka ya kiwanja ambacho Mahakama hiyo ya Haubi itakapojengwa. 

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA, Mahakama, Dar es Salaam)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni