Jumamosi, 6 Julai 2024

TANZIA; MTUMISHI MAHAKAMA YA MWANZO MATOMBO - MOROGORO AFARIKI DUNIA

Bw. Sospeter Mtindo Kuhoga enzi za uhai wake.

TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake, Bw. Sospeter Mtindo Kuhoga aliyekuwa akihudumu Mahakama ya Mwanzo Matombo iliyopo Wilaya ya Morogoro kwa nafasi ya Mlinzi Mkuu.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Bw. Ahmed Ng'eni amesema Bw. Kuhoga alifikwa na umauti jana tarehe 05 Julai, 2024 wakati akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.

Bw. Ng'eni amesema kwa sasa msiba upo Mazimbu karibu na Kitunda 'Bar' kwa binti yake. Ameongeza kuwa, maziko yatafanyika kesho tarehe 07 Julai, 2024 saa 10 jioni katika makaburi ya Kola yaliyopo Manispaa ya Morogoro.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu mzito wa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni