- ·Namba ya bure ya mrejesho
yatambulishwa kwa wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro
- Fomu maalumu za mrejesho
juu ya huduma za kimahakama zakabidhiwa kwa wafungwa na mahabusu gereza la
Karanga Moshi.
Na Paul Pascal-Mahakama
Moshi
Watumishi
wa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Mahakama ya Tanzania wamefanya ziara ya kikazi
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi pamoja na Gereza Kuu la Karanga Moshi
ikiwa ni ziara ya kuimarisha uhusiano na kuhimiza mrejesho wa huduma
zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania kwa njia ya maoni, malalamiko na mapendekezo
ya kuboresha huduma kwa mteja.
Akizungumza
mara baada ya kuwasili ofisi ya Mtendaji Mahakama Kuu Kanda ya Moshi mnamo
tarehe 28 Oktoba, 2024 Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Mahakama ya
Tanzania Bi. evetha Mboya aliieleza historia fupi ya uanzishwaji na lengo la
uanzishwaji wa kituo hicho.
“Kituo
chetu cha huduma kwa wateja kilianzishwa mwaka 2022 ikiwa ni utekelezaji wa
Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa mwaka 2020/21 had 2024/25 akatika
kutekeleza nguzo ya tatu ya urejeshaji wa imani kwa wananchi kikiwa na lengo la
kuwajumuisha na kuwashirikisha wananchi kupima huduma wanazopatiwa kama
zinafikia matarajio hayo. Ikilenga kuwapa wananchi fursa ya kutoa maoni, malalamiko
na mapendekezo juu ya huduma za kimahakama katika eneo linalowahudumia.”
alisema Bi. Mboya
Sambamba
na hilo watumishi hao kutoka Kituo hicho walipata wasaha wakuzungumza na
wananchi waliofika kwa ajili ya kupatiwa huduma za kimahakama katika Mahakama
Kuu Kanda ya Moshi, wajumbe huo ulifafanua huduma mbalimbali za Kituo hicho
ikiwemo kuwaelekeza matumizi ya namba ya simu inayotumika kutolea mrejesho wa
huduma kwa wateja pamoja na kuwaelimisha matumizi ya namba hiyo.
“Ndugu
zangu kituo chetu cha huduma kwa wateja tunayo namba ya simu kwaajili ya
kupokea maoni, malalamiko na mapendekezo juu ya huduma zinazotolewa na Mahakama
bila kujali ni Mahakama ya ngazi ipi na iko Mkoa gani au Wilaya gani. Kituo
kinapokea mrejesho wa huduma kwa Mahakama zote zilizopo Tanzania Bara kuanzia
ngazi ya Mahakama za Mwanzo, Mahakama za Wilaya, Mahakama za Hakimu Mkazi pamoja
na Mahakama Kuu zote kupitia namba za Bure bila malipo yoyote.” Alifafanua Bi.
Mboya.
Akizitaja
namba hizo za simu Mhe. Magesa Luponya alisema ni 0800750247 na whatsapp ni
0752500400. Kisha akawaomba wananchi wanapokuwa na haja ya kutoa mrejesho
wowote kutumia namba hizo kwa mawasiliano na Kituo ili watumishi wa Kituo hicho
kiwahudumie ipasavyo.
Ziara
hiyo ya siku moja ilihitimishwa kwa wajumbe hao kutembelea Gereza Kuu la
Karanga mjini Moshi nakuwapatia wafungwa na mahabusu fomu maalumu za mrejesho
wa huduma za Mahakama ili kuwawezesha kutoa maoni, malalamiko na mapendekezo juu
ya huduma zitolewazo na Mahakama ya Tanzania.
Afisa Utumishi Mwandamizi na Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja Bi. Evetha Mboya (mwenye suti nyeusi) pamoja na Mhe. Magesa Luponya (mwenye suti ya bluu ) akiongea na wateja waliokuwa fika Mahakama
Kuu Kanda ya Moshi.
Hakimu Mkazi Mhe. Magesa Luponya akitoa elimu kwa wananchi waliofika kupata huduma za kimahakama Mahakama Kuu Kanda ya Moshi.
Mwananchi akitoa hoja kuhusu huduma za kituo cha huduma kwa mteja cha Mahakama ya Tanzania.
Watumishi wa Kituo cha huduma kwa
wateja cha Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkuu wa
Gereza la Karanga Moshi baada ya kufanya ziara katika Gereza hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni