Na Daniel Sichula – Mahakama Mbeya
Mahakama
ya Wilaya Kyela, Kanda ya Mbeya imetoa elimu ya namna bora ya kutatua migogoro
itokanayo na biashara katika maonesho ya biashara na huduma za bidhaa
zinazozalishwa Ukanda wa Kusini mwa Afrika (Southern International Trade Fair and
Festival). Maonesho hayo yanayofanyika katika fukwe za Matema Beach wilayani Kyela
yalianza tarehe 21 Oktoba na kuhitimishwa tarehe 27 Oktoba 2024.
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya ikiwakilishwa na Mahakama ya Wilaya ya Kyela
ikatumia jukwaa hilo kutoa elimu ya namna bora ya kutatua migogoro ya
kibiashara, ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wadau juu ya shughuli mbalimbali za
huduma ya utoaji haki kwa wananchi kupitia mifumo ya kidijiti na kuainisha
malengo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama.
Akitoa
elimu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama Wilaya ya Kyela Mhe. Andrew
Severin Njau kwa kushirikiana na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Kyela
walijikita katika maeneo mbalimbali ikiwemo ufunguaji, uendeshaji na utatuaji
wa migogoro ya kibiashara kwenye Mahakama ya Biashara (Commercial Court) na
Mahakama za kawaida.
Aidha,
elimu hiyo pia iliangazia taratibu za ufunguaji na uendeshaji wa mashauri ya
mirathi na utatuzi wa migogoro inayoibuka maeneo ya kazi. Hiyo kupitia maonesho
hayo wadau mbalimbali walinufaika na elimu hiyo iliyotolewa na watumishi wa Mahakama
lengo ikiwa ni kujenga taswira chanya na kuimarisha imani ya wadau kwa Mahakama.
Ikiwa
ndiyo kwa mara ya kwanza maonyesho hayo ya kibiashara yanafanyika mkoani Mbeya,
jumla ya nchi saba za Kusini mwa Afrika zimeshiriki maonesho hayo ikiwemo
Rwanda, Zambia, Burundi, Malawi, Uganda, Kenya pamoja na mwenyeji Tanzania.
Sehemu ya wanafunzi waliotembelea banda la Mahakama katika maonesho hayo wakiwa na kiu ya kujifunza kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni