Na MWANDISHI WETU-Dar es Salaam
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda leo tarehe 14 Novemba, 2024 amemtembelea Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na kufanya naye mazungumzo mafupi.
Bw. Mwenda aliwasili ofisini kwa Jaji Mkuu iliyopo katika jengo la Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam majira ya saa 1.00 asubuhi, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya ziara hiyo tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo Julai, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akiwa na mwenyeji wake, Kamishna Mkuu wa TRA alijitambulisha rasmi kwa Jaji Mkuu na kumwomba kuendeleza ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Taasisi yake na Mahakama ya Tanzania.
Naye Mhe. Prof. Juma amemhakikishia Kamishna Mkuu huyo ushirikiano kwa kuzingatia Mamlaka ya Mapato nchini ni mdau muhimu kwenye jukumu la utoaji haki.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) na Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. George Herbert.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni