Na Daniel Sichula- Mahakama, Mbeya
Watumishi
wa Mahakama Mkoa Mbeya walikutana pamoja kwenye hafla ya kufunga mwaka
iliyofanyika tarehe 16 Novemba, 2024 katika Hoteli ya Lake Nyasa wilayani Kyela
mkoani Mbeya, hafla hiyo iliudhuliwa watumishi wa Mahakama Kuu, Mahakama ya
Mkoa, Mahakama za Wilaya na Mahakama za mwanzo.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya kufunga mwaka kwa watumishi wa Mahakama Mkoa wa Mbeya, Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga aliwahasa
watumishi wa Mahakama Mkoa wa Mbeya kufanya kazi kwa bidii na kutoa tathimini
ya utendaji kazi kwa Mahakama zote katika kushughulikia mashauri.
“Tunapoelekea
kufunga mwaka, napenda kuwapongeza Majaji kwa kuongoza na kupunguza mashauri
tuliyokua nayo kwa muda mfupi na mpaka sasa mafanikio makubwa yamefanyika kwani
tumevuka kiwango cha asilimia 50 kwa kumaliza mlundikano wa mashauri katika Mahakama
zetu, hata hivyo nazipongeza Kada zote kwa ufanisi katika utendaji kazi kwa
Mahakama zote” alisema Mhe. Tiganga
Aidha,
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi. Mavis Miti alisema, “Lengo la hafla
hii ni kufurahi kwa pamoja na kuweza kufamihana kwa watumishi wa Mahakama Mkoa
wa Mbeya kwani kuna wengine ni wageni kabisa, kwa hiyo hii ni fursa pekee ya
kuweza kufahamiana kwa viongozi na watumishi kwa ujumla vilevile kupongezana
kwa utendaji mzuri wa kazi katika Mahakama zetu,” alisema Bi. Miti.
Watumishi
mbalimbali kutoka Mahakama za Mkoa wa Mbeya walitoa pongezi kwa uongozi wa Mahakama
Mkoa wa Mbeya kwa kuweza kuwaleta pamoja watumishi wote wa Mahakama Mkoa Mbeya
na kufanikisha hafla hiyo ambayo imekua chachu kwao ili kufanya kazi kwa bidii
na kufikia malengo waliyojiwekea.
“Tunahidi
kufanya kazi kwa bidii baada ya kutoka kwenye hafla hii ambayo imekuwa imetupa
hamasa ya kazi, tumeshiriki kwa pamoja katika burudani mbalimbali zilizotuondolea
msongo wa mawazo na kujenga akili mpya katika utendaji kazi,” alisema mmoja wa
watumishi hao
Aidha,
hafla hiyo iliudhuliwa na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya
Mhe. Aisha Sinda na Mhe. Musa Pomo, Naibu Msajili Mhe. Judith Lyimo, Mahakimu Wafawidhi,
Mahakimu wa Mahakama za Wilaya na Mwanzo, Mawakili, Maafisa wa Vitengo
mbalimbali na watumishi wa Kada mbalimabali kutoka Mahakama Kuu Mbeya.
Watumishi wa Mahakama Mkoa Mbeya waliokutana pamoja kwenye hafla ya kufunga mwaka iliyofanyika tarehe 16 Novemba, 2024 katika Hoteli ya Lake Nyasa wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akisema jambo wakati wa hafla hiyo.
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama Mkoa Mbeya waliokutana pamoja kwenye hafla ya kufunga mwaka
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama Mkoa Mbeya waliokutana pamoja kwenye hafla ya kufunga mwaka.
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama Mkoa Mbeya waliokutana pamoja kwenye hafla ya kufunga mwaka
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama Mkoa Mbeya waliokutana pamoja kwenye hafla ya kufunga mwaka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni