Jumapili, 15 Desemba 2024

ASKARI JESHI PANGAWE WATEMBELEA IJC MOROGORO

Na EVERINE ODEMBA – Mahakama, Morogoro

 Askari 85 kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania walioko kwenye Shule ya Mafunzo ya Huduma na Utawala kutoka Kituo cha Mafunzo cha Kijeshi Pangawe mkoani hapa wamefanya ziara ya mafunzo katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Morogoro ili kupata uelewa wa Mahakama na mifumo yake.

 Ziara hiyo ilifunguliwa na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Amir Mruma ambaye hakusita kuonesha furaha yake kwa ugeni huo huku akiwahakikishia kuwa mara watakapohitimisha ziara yao watakuwa wamekidhi kiu yao ya kutaka kujifunza kuhusu Mahakama.

 “Kuja kujifunza hapa ni sehemu sahihi kabisa kwa sababu Mahakama ya sasa imepiga hatua madhubuti kimaboresho kuanzia namna ya usikilizaji wa mashauri na hata kuwepo kwa miundombinu rafiki ambayo imezingatia makundi yote ikiwemo wenye mahitaji maalum,” alisema Mhe. Mruma.

Aliongeza kuwa timu ya wataalamu toka Mahakama Morogoro imejipanga vyema kutoa elimu kwa askari hao, hivyo aliwaomba mara baada ya ziara yao wawe mabalozi wazuri wa kuitangaza Mahakama na kuelezea maboresho makubwa yaliyofanyika.

Mhe. Mruma alifafanua kuwa anatambua kuwa kuna Mahakama za Kijeshi na zinafanya kazi, hivyo aliwataka wanajeshi hao kubadirishana uzoefu na watoa maada ya namna wanavyofanya katika Mahakama ya Kijeshi kwa kuwa lengo ni wote kujengeana uelewa wa pamoja.

“Napenda kumshukuru Mkuu wa Chuo cha JWTZ Pangawe kwa hamasa hii na tunamuahidi ushirikiano bora na imara wa lengo la kujengeana uelewa wa pamoja,” alisema na kuongeza kuwa Mahakama Kanda ya Morogoro inajivunia ujio wa Askari hao na hamasa kubwa wanayoionesha ya kutaka kujifunza.

Naye Kiongozi wa Askali hao, Kapteni Yona Mtaita alisema kuwa msafara huo una jumla ya Askari Jeshi 85 na sita kati yao ni Wakufunzi na Askari 79 ni Wanafunzi wanaoendelea na mafunzo katika Shule ya Mafunzo ya Huduma na Utawala toka katika Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi Pangawe.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Amir Mruma akizungumza na Askari Jeshi toka Shule ya Mafunzo ya Huduma na Utawala Pangawe (hawapo pichani). Kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Morogoro,  Bw. Ahmed Ng’eni na kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Morogoro, Mhe. Mary Kallomo.

Meza Kuu ikiongozwa na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Mhe. Amir Mruma (aliyevaa tai nyekundu) ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Askari Jeshi waliofanya ziara ya kimafunzo katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Morogoro.

 

Meza Kuu ikiongozwa na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Mhe. Amir Mruma (aliyevaa tai nyekundu) ikiwa katika picha ya pamoja na Wakufunzi toka Shule ya Mafunzo ya Kijeshi Pangawe.

 Meza Kuu ikiongozwa na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Mhe. Amir Mruma (aliyevaa tai nyekundu) ikiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu toka Kanda ya Morogoro ambao ndio timu iliyoandaliwa kutoa elimu kwa Askari hao.

 

 Meza Kuu ikiongozwa na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Mhe. Amir Mruma (aliyevaa tai nyekundu) ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Askari Jeshi wanawake waliokuwa kwenye ziara hiyo.

Askari Jeshi toka Shule ya Mafunzo ya Huduma na Utawala Pangawe wakifuatilia mada ndani ya Ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Morogoro wakati walipofanya ziara yao kituoni hapa.

 (Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni