- Asisitiza Uadilifu, Weledi, Uwajibikaji
Na
ARAPHA RUSHEKE –Mahakama, Dodoma
Kaimu Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Edwin Elias Kakolaki amewataka watumishi ajira mpya
ambao wamejiriwa na Mahakama ya Tanzania hivi karibuni kuishi katika salaam ya
Mahakama inayohimiza uadilifu,weledi na uwajibikaji.
Akizungumza
na watumishi hao juzi tarehe 18 Disemba,2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo
katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma, Mhe. Kakolaki aliwataka kufanya
kazi kwa weledi na bidii ili kuhakikisha mpango mkakati wa Mahakama unafikiwa
kwa kiwango kikubwa.
Aidha, Kaimu
Jaji Mfawidhi huyo aliwakaribisha pia watumishi wapya na kuwasihi kuishi katika
maadili ya utumishi wa umma pamoja na kupenda kujifunza kazi Zaidi, kwani
kufanya hivyo kutawarahisishia na kumaliza majukumu yao kwa wakati.
“Nimefarijika kuwaona na nina wakaribisha sana
katika Kanda hii ya Dodoma. Nina imani mtafanya kazi kwa weledi na uadilifu
kama ambavyo viapo vyenu vinavyosema. Hakikisheni
mnaiishi salamu ya Mahakama ambayo inasema uadilifu, weledi na uwajibikaji,
ninahakika mkiishi salamu hiyo mtafanya kazi kwa uadilifu mkubwa sana,” alisema.
Kwa upande
wake, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Silivia Selestine
Lushasi aliwapongeza na kuwakaribisha watumishi hao na kuahidi kushirikiana nao
katika kazi. Alitumia wasaa huo kuwahimiza kuzingatia uadilifu na maadili
katika kazi zao kwa kujiepeusha na matendo yote ambayo yataharibu haiba ya
uadilifu wao.
Naye Mtendaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Bw. Sumera Manoti aliwataka watumishi hao
wakatimize wajibu wao kwa mujibu wa sharia, taratibu na miongozo.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Edwin Elias Kakolaki akizizitiza jambo wakati wa kikao na watumishi wapya kilichofanyika katika ukumbi wa IJC Dodoma.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Silivia Selestin Lushasi akiongea jambo wakati wa kikao hicho.
Meza Kuu wakiongozwa na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Mhe. Edwin Elias Kakolaki (aliyekaa katikati)kulia kwake ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Mhe.Silivia Selestini Lushasi na kushoto kwake ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Dodoma, Bw .Sumera Manoti wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wapya pamoja na watumishi wengine wa Mahakama waliohudhuria kikao hicho.
Mtendaji wa
Mahakama Kuu Dodoma, Bw. Sumera Manoti (aliyekaa katikati), kushoto kwake ni
AfisaUutumishi Mwandamizi wa Mahakama Kuu Dodoma, Bw. Stanley Makendi, kulia
kakwe na Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mahakama Kuu Dodoma, Bi. Doto Sosela, walio
simama kulia kwake ni Afisa Tawala Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya Kondoa, Bi.
Edna Dushi na anayefuatia ni Afisa Utumishi wa Mahakama ya Wilaya Bahi, Bi.
Recho Lubeleje.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni