Jumamosi, 21 Desemba 2024

MAJAJI MAHAKAMA YA RUFANI WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA MAHAKAMA, NYUMBA ZA MAJAJI

Na ARAPHA RUSHEKE –Mahakama, Dodoma

Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania jana tarehe  20 Desemba, 2024 walitembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania na  kupongeza hatua kubwa iliyofikiwa.

Baada ya kuwasili katika jengo hilo, Majaji hao, Mhe. Augustine Gherabast Mwarija, Mhe. Rehema Kiwanga Mkuye, Mhe. Dkt Gerald Mbonipa Ndika na Mhe. Leila Edith Mgonya walipata fursa ya kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali za kiutendaji zinazoendelea.

Wakiwa katika ukumbi wa mkutano, Majaji hao walipata taarifa mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Moses Lawrence Lwiva juu ya Jengo hilo lililopo eneo la Tambukareli na baadaye kutembelea ofisi mbalimbali katika jengo hilo.

Walionesha kufurahishwa na uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama  na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kufanikishakazi hiyo.

Majaji hao walipata fursa pia ya kutembelea eneo la makazi ya Majaji lililopo eneo la Iyumbu na NCC jijini Dodoma.

"Tunaishukuru sana Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama na makazi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu. Tunaamini Majaji watafanya kazi wakiwa katika mazingira rafiki yanayoendana na kazi zao,"alisema Mhe. Mwarija.

Viongozi wengine wa Mahakama waliombatana na ugeni huo ni Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Bw. Victor Florence Kategere, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Bi. Beatrice Patrick pamoja na watumishi wa Mahakama ya Tanzania.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Augustine Gherabast Mwarija, (aliyekaa mbele katikati), wa kwanza kushoto kwake ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Rehema Kiwanga Mkuye, wa kwanza kulia kwake ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt Gerald Mbonipa Ndika anayefuatia kushoto kwake ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Leila Edith Mgonya (alievaa miwani) na wa pili kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Bw. Victor Florence Kategere wakipata maelezo mafupi na taarifa mbalimbali kutoka kwa Mhandisi (hayupo pichani ) Bw Moses Lawrence Lwiva katika ukumbi wa mkutano uliopo katika ofisi ya Mahakao makuu ya Mahakama Jijini Dodoma.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Augustine Gherabast Mwarija akisikiliza kwa makini taarifa kutoka kwa Mhandisi, Bw. Moses Lawrence Lwiva (hayupo pichani)

Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakiwa katika moja ya ofisi ya Jaji wa Mahakama ya Rufani mara baada ya kutembelea ofisi hizo zilizopo katika Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma.

Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya rufani pamoja na watumishi wa Mhakama wakiwa katika picha ya pamoja.

Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Augustine Gherabast Mwarija, (wa kwanza kulia) kushoto kwake  ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe.Dkt Gerald Mbonipa Ndika wakiwa katika picha ya pamoja katika moja ya nyumba za makazi za Majaji zilizopo eneo la Iyumbu Dodoma.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Augustine Gherabast Mwarija, (wa kwanza kulia ) aliyeshika kiti akisiliza kwa umakini maelezo kutoka kwa Mhandisi, Bw.Moses Lwiza (hayupo pichani ) mara baada ya kufika katika nyumba za makazi ya Majaji zilizopo eneo la Iyumbu.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Augustine Gherabast Mwarija akiwa katika sehemu ya makazi ya nyumba za Majaji wa Mahakama ya Rufani zilizopo Iyumbu Dodoma.

Sehemu ya viongozi na watumishi walioambatana na ugeni huo wakisiliza kwa makani maelekezo.

Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani pamoja na watumishi wa Mahakama wakiingia katika nyumba za Majaji wa Mahakama ya Rufani eneo la Iyumbu Jijini Dodoma.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni