Na ASHA JUMA-Mahakama Morogoro.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Aisha Sinda hivi karibuni aliendesha kikao cha maandalizi na mikakati ya namna ya kusikiliza mashauri ya jinai ndani ya muda mfupi.
Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Morogoro kilihusisha Wadau mbalimbali, wakiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Polisi, Mkuu wa Magereza na Mawakili wa Kujitegemea.
Katika Kikao hicho, wajumbe walikubaliana kuwa mashauri hayo yataanza kusikilizwa kuanzia leo tarehe 10 Machi, 2025 hadi tarehe 10 Aprili, 2025.
Mwenyekiti wa Kikao hicho aliwataka Wadau wawe na ushirikiano na kuandaa mashahidi wao vizuri.
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Nicolaus Lupa alisema kuwa kwa kuwa wamepata wito mapema watajitahidi kuandaa mashahidi na kutatua changamoto zinazowakabili ili kufikia lengo.
Kwa upande wa mwakilishi wa Mkuu wa Magereza, SP Sabasaba Mselem alisema kuwa wataendelea kuhifadhi Mahabusu kulingana na orodha ya kesi husika.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Aisha Sinda akizungumza wakati wa kikao hicho.
Wadau na wajumbe wa Mahakama-juu na chini-wakiwa kwenye kikao.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni