Na ARAPHA RUSHEKE-Mahakama Kuu, Dodoma
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma. Mhe. Dkt. Juliana Masabo leo tarehe 27 Machi, 2025 ameongoza Kikao cha Baraza la Wafanyakazi Kanda ya Dodoma kujadili mambo mbalimbali ya kikazi.
Akizungumza wakati anafungua Kikao hicho ambacho kilimefanyika katika Ukumbi wa Mahakama ya Wilaya Mpwapwa, Mhe. Dkt. Masabo amewapongeza Watumishi wote kutokana na kazi nzuri wanazozifanya katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Hata hivto, Jaji Mfawidhi ameiwataka wajumbe wa Kikao hicho pamoja na uongozi wa Kanda kuhakikisha kwamba Watumishi wote wanapata mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHAMA- kazini.
“Ukisoma nyaraka zetu za maboresho tunazungumzia kuifikisha Mahakama ya Tanzania katika hadhi ya e-judiciary, yaani Mahakama inayotoa huduma zote za haki na zinazowezesha utoaji haki kufanyika kwa njia ya mtandao. Viongozi tunayo wajibu na jukumu la kuendelea kuwahimiza Wafanyakazi na Watumishi wote wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi katika mazingira ya Mahakama Mtandao,’ alisema Dkt.Masabo.
Sanjari na hayo, alinukuu maneno ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani aliyoyasema tarehe 19 Machi, 2025 alipokuwa jijini Mwanza katika kikao cha Majaji Wafawidhi.
Katika kikao hicho, Jaji Kiongozi alihimiza Majaji kuzidisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA ili kufanikisha azma ya Mahakama ya Tanzania ya kuachana na karatasi katika shughuli zote za kimahakama.
‘Nami natoa maelekezo kwa Viongozi wote wa Mahakama Kanda, kuhakikisha kwamba matumizi ya TEHAMA yanaendelea kutumiwa katika nyanja zote za shughuli za Mahakama kila siku,’ alisema.
Katika Kikao hicho, mada mbalimbali zilijadiliwa, huku Jaji Mfawidhi akieleza kuwa Baraza hilo ni muhimu kwa sababu ni chachu ya mahusiano mazuri baina ya uongozi na watumishi katika maeneo yao ya kazi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza, Mhe. Dkt. Juliana Masabo akiwa katika Ofisi ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Mpwapwa kabla ya kuanza kikao hicho.
Msaidizi wa Sheria wa Jaji ambaye pia ni Katibu wa kikao hicho, Mhe. Gerald Gamba-aliyesemama-akitoa neno la ukaribisho.
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakiiimba wimbo wa mshikamano daima.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza, Mhe. Dkt. Juliana Masabo akisisitiza jambo.
Sehemu ya wajumbe wa baraza kutoka Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa umakini.
Sehemu ya wajumbe wa baraza kutoka Dodoma wakifuatilia kwa umakini.
Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza, Mhe. Dkt. Juliana Masabo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Mkoa wa Singida. Waliokaa kulia kwake ni Katibu wa kikao hicho, Mhe. Gerald Gamba na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tughe Mkoa wa Dodoma, Bw. Maulidi Kipeneku.
Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza, Mhe. Dkt. Juliana Masabo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Mkoa wa Singida. Waliokaa kulia kwake ni Katibu wa kikao hicho, Mhe. Gerald Gamba na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tughe Mkoa wa Dodoma, Bw. Maulidi Kipeneku.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni