Na
Mwinga Mpoli- Mahakama, Mbeya
Katika kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Majaji na Mahakimu wanawake walitumia
siku hiyo ya jana tarehe 10 Machi, 2025 kutoa elimu katika shule mbalimbali za Msingi
na Sekondari za jiji la Mbeya.
Aidha,
Shule zilizotembelewa katika zoezi hilo la utoaji elimu ni pamoja na Sangu High
School, Samora Michel High School zilizopo katika Wilaya ya Mbeya na kutoa elimu
kwa wanafunzi takribani 100,000 kutoka kwa waheshimiwa Majaji na Mahakimu Wanawake.
Waheshimiwa
hao walitoa mada zilizoandaliwa na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake
Tanzania (TAWJA) zenye lengo la kuelimisha umma juu ya haki za msingi katika
zama za kidigitali, huku wakifafanua mchango wa Majaji na Mahakimu Wanawake
katika kushughulikia makosa ya unyanyasaji wa kimtandao kwa jinsia zote.
Waheshimiwa
waliyoshiriki kutoa elimu hiyo walikuwa Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Mhe. Atuganile Ngwala, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe Zawadi Laizer, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mwanjelwa Mhe. Angela
Kannyaninyi Byera, Mhe. Joyce Massawe, Hakimu mkazi mahakama ya Mwanzo
Mwanjelwa, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Iyunga Mhe. Hafsa Shelimo na Hakimu
Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini Mhe. Miriam Kamwaga.
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Atuganile Ngwala (aliyevalia Gauni ya Kitenge) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waheshimiwa Mahakimu Wanawake na pia Uongozi wa Shule ya Sekondari Samora Michel iliyoko jijini Mbeya mara baada ya kutoa elimu katika Siku ya Kimataifa ya Majaji na Mahakaimu Wanawake.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe. Zawadi Laizer akitoa mada kuhusu adhabu zinazoweza kutolewa kwa mkosaji wa makosa ya kimtandao.
Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Iyunga Mhe. Hafsa Shelimo akitoa mada kuhusu
majukumu ya polisi kwenye upelelezi wa makosa ya kimtandao.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni