Jumanne, 25 Machi 2025

MENEJIMENTI MAHAKAMA KANDA YA DAR ES SALAAM YAFANYA KIKAO

Na EUNICE LUGIANA-Mahakama, Pwani

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi amewataka Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama zote kwenye Kanda hiyo kuwa wabunifu katika kusikiliza mashauri ili kuondokana na mlundikano.

Mhe. Maghimbi alitoa wito huo hivi karibuni alipokua akifungua kikao cha menejimenti cha Mahakama Kanda ya Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani.

Aliwahimiza kuendesha kesi kwa njia ya mtandao, hata kama hawaonani bali Hakimu ajiridhishe kwamba anayeongea naye ndio mhusika.

Jaji Mfawidhi alisema kuwa Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi Kisutu na Kinondoni kuondoa dhana ya kwamba Mahakama hizo haziwezi kuondoa kesi zote za mlundikano.

“Kumekuwa na dhana kwamba kesi ni nyingi na haziwezekaniki, hiyo ni dhana tu ambayo pia ilikuwepo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Sasa mashauri hayo yamepungua kama siyo kuisha kabisa,” alisema Mhe. Maghimbi.

Kadhalika, Jaji Mfawidhi waliwataka Viongozi hao kusimamia rasilimali za Mahakama, hasa majengo mapya ili yabaki katika ubora wake.

Katika kikao hicho, Mhe. Maghimbi pia aliwakumbusha wajumbe kuwa   ukaguzi wa Magereza ufanyike mara kwa mara na sio kusubiri mpaka kutembelea, kwani Mahabusu wengine hawawezi kuongea pindi wakitembelewa.

Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Wafawidhi hao kwa kuafanya vizuri kwenye mashauri kutoka katika mlundikano wa mashauri uliokuwepo awali kwani jitihada kubwa imefanyika.

Katika kikao hicho, wajumbe waliadhimia kwamba kila Mahakama ya Mwanzo iwe na rejista ya kuandika matukio yote yanayotokea kwa siku kama kuna mtu kaja kutaka huduma yoyote.

Pia waliadhimia kila Hakimu Mfawidhi akague akaunti yake ya mirathi ili kujua kama kuna fedha ambazo hazijalipwa ili zilipwe kwa wahusikana na kama wahusika hawajulikani watafute kwa namna yoyote ili waweze kulipwa.

Azimio lingine ni kwamba kwa mahakama ambazo zimekuwa na mlundikano  wa mashauri kuondoa dhana hiyo na hatua za makusudi zichukuliwe.

Kikao hicho kilihudhuliwa na Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za Wilaya, Watendaji, Maofisa Utumishi na Maafisa Tawala, Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani,  Maofisa TEHAMA, Mafundi Sanifu, Ofisa Kumbukumbu na Wasaidizi wa Kumbukumbu wa  Kanda ya Dar es Salaam.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi na Mwenyekiti akifungua kikao hicho.

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Moses Mashaka, ambaye ni Katibu wa kikao hicho akisoma agenda.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (katikati), kushoto ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe Mary Moyo na kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Moses Mashaka.

Wajumbe wa menejimenti wakiendelea na kikao.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi akibadilishana mawazo na  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe Abubakar Kunenge.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni