Na NAOMI KITONKA-Mahakama, Kituo Jumuishi Temeke.
Mafunzo
ya siku tatu kuhusu
Kuepuka Kutonesha Majeraha kwa Waathirika na Mashahidi wa Ukatili wa Kijinsia
na Kingono (SGBV) kwa Mahakimu Wakazi, Waendesha Mashtaka, na Maafisa Ustawi wa
Jamii yamefungwa jana tarehe 16 Aprili 2025 na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Famila – Temeke, Mhe.
Gladys Barthy.
Katika
kuhitimisha mafunzo hayo yaliyokuwa
yanafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano kwenye Kituo hicho, Mhe.
Barthy alisisitiza umuhimu wa kila mshiriki wa mafunzo kuwa chachu ya kuyatenda
yale waliyojifunza kwa vitendo na pia kubadilishana uwezo na Watumishi wengine, hasa linapokuja suala la kuwahudumia
wahanga na waathirika wa ukatili.
“Siku
hizi chache zenye mafunzo mengi na kubadilishana uzoefu kusiwe bure, kwa
uchache wetu tujitahidi kama W,atumishi
wa Mahakama kuhakikisha tunakuwa watu wa kwanza kuwalinda walio hatarini na
kuepusha kuwarejeshea majeraha yatokanayo na ukatili wa kingono na kijinsia ili
tuwe mfano bora wa kuigwa” aliongea Mhe. Barthy.
Akitoa
neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wengine, Mhe. Mhangwa Yunge alisema kuwa mafunzo hayo yamewabadilisha mtazamo na kuweka
alama ya namna ambavyo,
kama watu wenye dhamana ya kutoa haki,
wanapaswa kuwasaidia waathirika wa unyanyasaji na mchango mkubwa walionao
katika kuwaondolea woga wa taratibu za kimahakama.
Naye Mkurugenzi wa Mafunzo ya Kimahakama
wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Mhe. Dkt. Patricia Kisinda, akizungumza katika hafla hiyo, alisema,
“Tunawashukuru wote kwa kushiriki na mafunzo haya yamekuwa ya vitendo zaidi na
tumeona mafanikio ya yale mengi ambayo tumefundishwa mahali hapa na sisi tukawe
mabalozi wazuri katika vituo vyetu vya kazi,
kuhakikisha ujuzi na maarifa haya adhimu
yanaleta matokea chanya katika utendaji wetu na jamii kwa ujumla.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni