Na MUSSA MWINJUMA-Mahakama Kuu Tanga
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tanga, Mhe. Katarina Revocati
Mteule hivi karibuni aliongoza Baraza la Wafanyakazi kwenye Kanda hiyo kujadili
mambo mbalimnbali ya kiutendaji.
Akifungua mkutano wa Baraza hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Wazi wa Mahakama Kuu Tanga,
Mhe. Mteule aliwashukuru wajumbe wote kufika kwa wakati pamoja na kwamba
wengine wanatoka mbali.
Mhe.
Jaji Katarina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo aliwakumbusha wajumbe umuhimu
wa uwepo wa Baraza hilo kwani ni jukwaa la kujadili mambo mbalimbali muhimu yanayowahusu
wafanyakazi.
“Baraza la Wafanyakazi ni chombo ambacho
wajumbe hutoa maoni, ushauri, mapendekezo na hata kukosoa kwa niaba ya Watumishi
wengine ambao hawako hapa ili michango hiyo iingie kwenye utekelezaji wa
shughuli za Mahakama, usiwe hapa kwa ajili ya kuongea matatizo yako binafsi ya
kiutumishi,” alisema
Naye
Afisa Kazi, Bw. Juma Mkali aliwapitisha wajumbe kwenye umuhimu,d humuni la mabaraza
ya wafanyakazi. Pia aliwapitisha katika sheria mbalimbali za uundwaji wa
mabaraza na kazi zake, ikiwemo ushauri juu ya maslahi ya wafanyakazi, utaratibu
wa vyeo na nidhamu, kupokea na kujadili mapato na matumizi ya Taasisi.
Katika
mkutano huo kulifanyika uchaguzi wa Katibu na Naibu Katibu kwa mujibu wa sheria
za uundwaji wa baraza zinavyotaka ambapo Bw. Alinani Mwaiswelo alichaguliwa kuwa
Katibu na Mhe. Bahati Manongi akiwa Naibu Katibu. Naye Bw. Farid Mnyamike ambaye
ni Afisa Utumishi wa Kanda hiyo alichaguliwa kuwa mwakilishi wa Wafanyakazi
katika Baraza la Wafanyakazi Taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni