Na MWANAIDI MSEKWA na NAOMI KITONKA- Mahakama, Dar es Salaam.
- Kiwango uondoshaji mashauri kimepanda mwaka 2024.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Prof. Ibrahim Hamisi Juma leo tarehe 24 Aprili 2025 ameongoza kikao kazi cha tathmini ya shughuli za Mahakama ya
Rufani kwa mwaka 2024.
Kikao
hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Julius Kambarage
Nyerere, Dar-es Salaam
kiliambatana na uwasilishaji wa Taarifa ya Mashauri kwa kipindi cha Januari
hadi Disemba 2024 iliyowasilishwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. George Herbert pamoja na taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya kiutawala
na kiutumishi kwa mwaka 2024/2025 iliyowasilishwa na Mtendaji wa Mahakama ya
Rufani, Bw. Victor Kategere.
Akiongea
katika taarifa hiyo, Mhe. Herbert alisema takwimu zinaonyesha idadi ya mashauri
yanayoondolewa ni kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja kulinganisha na kipindi
kilichopita cha mwaka 2023,
japokuwa mzigo wa mashauri umeongezeka kwa
mwaka 2024.
Alisema pia kuwa Mahakama ya Rufani imeendelea
kusikiliza mashauri kwa njia ya mtandao kwenye vikao vya majopo, maombi ya
faragha, usomaji wa maamuzi na usikilizaji wa maombi ya madai ya gharama za
kesi (taxations).
Kadhalika, Mahakama imeendelea kupandisha kwa wakati
maamuzi yote yanayopaswa katika tovuti ya TanzLII na kuanzia mwezi Februari
mwaka 2025 Mahakama ya Rufani imeanza rasmi matumizi ya mfumo wa eCMS kuanzia
kufungua shauri hadi kusomwa hukumu.
Pia
taarifa iliyowasilishwa na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani iligusia maeneo muhimu ya vipaumbele
vilivyowekwa na Mahakama hiyo,
yakiwemo mkakati wa kuharakisha utatuzi wa mashauri ya kawaida, uendeshaji wa
vikao vya Mahakama (Session), matumizi ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano -TEHAMA Pamoja na kuongeza
ushirikiano na wadau wa haki jinai.
“Pamoja
na mafanikio haya, Mahakama ya Rufani imedhamiria kuharakisha utatuzi wa mashauri ya kawaida na mkakati wa
kumaliza mashauri ya muda mrefu, kuboresha mifumo na matumizi ya TEHAMA, kuimarisha uwezo katika ukaguzi na usimamizi wa shughuli
za Mahakama, kuendelea kutekeleza mpango wa ujenzi na ukarabati wa majengo
ya Mahakama, kuongeza ushirikiano na wadau wa haki jinai pamoja na kuimarisha
maendeleo ya rasilimali watu ikijumuisha mafunzo na nidhamu ya watumishi wetu,”
aliongeza Bw. Kategere.
Aidha, alihitimisha kwa kusisitiza kuwa Mahakama ya
Rufani itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na wadau wa ndani
na nje ili kuhakikisha haki inaendelea kutolewa kwa wakati. Aidha, ili
kuwafikia wananchi kwa wakati, Mahakama itaendelea kuimarisha na kuboresha matumizi
ya TEHAMA katika huduma mbalimbali zitolewazo na Mahakama.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na Majaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi, Msajili Mkuu,
Mtendaji Mkuu, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Naibu Wasajili, Wakurugenzi,
Wasaidizi wa Sheria na Watumishi
wa kada mbalimbali za Mahakama.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani na Jaji wa Mahakama Kuu na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Mahakama ya Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wasajili wanaohudumu katika Mahakama ya Rufani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni