Na MAGRETH KINABO- Mahakama, Dodoma
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kwamba Mahakama ya Tanzania haifanyi biashara bali inatoa huduma ya utaoaji ya haki kwa Wananchi, ndio maana Serikali imewekeza rasilimali fedha ya kiasi cha Sh. bilioni 416.16 kwa ajili kuboresha miundombinu ya Mahakama nchini katika kipindi cha miaka minne.
Aidha amesema kuwa fedha hizo, zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa wakati akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha jukumu la utoaji haki linatekelezeka.
Ahadi hiyo, ilitolewa na Rais Dkt. Samia mara baada ya kushika wadhifa huo wa juu zaidi hapa nchini, tarehe 19 Machi, 2021 jijini Dodoma.
Prof. Ole Gabriel amesema hayo, leo tarehe 5 Aprili, 2025 wakati akitoa taarifa ya miradi yote iliyotekelezwa kwa kipindi hicho, kwa Rais Dkt. Samia.
“Fedha hizi ni jumla ya miradi yote iliyotekelezwa na keendelea kutekelezwa ikiwemo mradi wa ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania lililopo jijini Dodoma, ambapo ndio Makao Makuu ya Nchi.Mradi mwingine ni Ujenzi wa Makao Makuu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama yote imejengwa eneo la Tambuka Reli na mradi wa Makazi ya Majaji, ambayo yamejengwa kwa mtindo wa block mbili zenye nyumba 48, yapo eneo la Iyumbu, jijini Dodoma,”amesema Prof.Ole Gabriel.
Majengo hayo ya Mahakama ambayo matatu yamezinduliwa leo na Rais Dkt. Samia ambaye alikuwa mgeni rasmi yaliyogharimu Sh.bilioni 185.4, ambazo ni fedha za walipakodi ambao ni Watanzania.
Akizungumzia kuhusu Jengo la Makao Makuu ya Mahakama, amesema ni la kisasa na kimataifa , pia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025 na lina ngazi 31 ambazo zinahakisi kuwa ni eneo la Mamlaka na limegharimu Sh. bilioni 129.7. pia lina hekari 12 kwa shamba la kawaida na linachukua watumishi 780 wa makao hayo.
“Jengo hili lina Chumba Maalumu cha kisasa chenye Mifumo 17 ya Teknolojia Habari na Mawasiliano(TEHAMA) ya Kutolea Taarifa mbalimbali za Kimahakama nchi nzima(JSR) iliyojengwa na wataalamu wa ndani ya nchi ,Kituo cha Huduma kwa Mteja, Mahakama za Wazi 10, kumbi ndogo 22 zenye uwezo wa kuchukua watu kuanzia 15,30,50,85, na Faragha, Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wenye uwezo kuchukua watu 346, mita za mraba 63, 244 lina sehemu ya utawala... mabwawa ya kuogelea,
“Afrika na dunia ifahamu kuwa jengo hili linashika nafasi ya sita kwa majengo ya Makao Makuu ya Mahakama Duniani kwa ukubwa na lina sakafu tisa, ni la kwanza Barani Afrika”amesisitiza.
Kuhusu Makazi ya Majaji amesema kuwa hivi sasa Majaji wameshahamia kwenye nyumba hizo, ambazo zina mifumo ya usalama, maegesho ya magari, huduma za mtandao ili kuboresha mazingira ya kazi.
Ameongeza kuwa fedha zingine zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki (IJC) sita vya awamu ya kwanza na vingine tisa vya awamu ya pili vinavyoendelea kujengwa, ambapo kimoja kiko Pemba. Fedha ujenzi wa vitro hivyo ni mkopo wa gharama nafuu kutoka Benki ya Dunia (WB).
Nyingine ni baadhi ya Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo na kukarabati majengo ya Mahakama Kuu mbili ili ziwe Mahakama za Familia ambazo ni iliyokuwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akati akitoa taarifa ya miradi yote iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa upande wa Mhimili wa Mahakama katika kipindi cha miaka minne kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakiwemo wageni wengine waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Majengo Matatu ya Mahakama yaliyopo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo tarihe 5 Aprili, 2025 katika Viwanja vya Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania vilivyopo eneo la Tambuka Reli jijini hapa, ambapo ndipo Makao Makuu ya Nchi na kuandika historia, kwamba Mihimili Mitatu ya Dola sasa imehamia Dodoma.
Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.
Kwaya ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baadhi ya Majaji na wageni waalikwa, wakiwemo Viongozi Waandamizi kutoka Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani, ambaye Pia alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kwanza wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga(aliyekaa) akisalimia na mmoja wageni waliohudhurio hafla hiyo na kushangiliwa baadhi ya yatu kutokana na uwepo wake na utendaji kazi mzuri katika Mhimili huo wa Mahakama.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakisalimiana na Mawaziri mara baada ya kuingia katika Viwanja vya Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya TanzaniaTanzania wakifualitia hafla hiyo.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakifualitia hafla hiyo.
Baadhi ya Mawaziri na wageni waalikwa waliohudhuria.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, ambaye Pia alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kwanza wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga(kushoto) akiwa na Mtendaji Mkuu wa pili wa Mhimili wa Mahakama, Bw. Mathias Kabunduguru(katikati).
Viongozi wa dini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akikagua funguo wa dhahabu wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassa, akimkabidhi Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma funguo wa dhahabu wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitoa maelekezo ya utunzaji wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma mara baada ya kukabidhi funguo wa huo.
Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Mkuu wa Zanzibar wakiwa wanasubiri tukio la kukabidhi funguo za majengo hayo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Kevin David Mhina akizungumza jambo na Mtendaji Mkuu wa pili wa Mhimili wa Mahakama, Bw. Mathias Kabunduguru.Picha za juu na chini.
Baadhi ya Watendaji wa Mahakama za Kanda mbalimbali.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini makala malum ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kuhusu mageuzi yaliyofanywa na Mahakama.
Picha za juu na chini ni viongozi wa dini wakimwombea dua Rais, na wasaidizi wake, likiwemo tukio hilo.
Picha za chini ni kikundi ni cha ngoma ya kibati kutoka Zanzibar kikitumbuiza nyimbo za kumpongeza Rais kwa utendaji wake wa kazi kutaja sofa za Majengo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mhe. RoseMary Senyamule akisalimiana na Baadhi wa Viongozi wa Serikali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
Mhe. William Vangimembe Lukuvi Akizungumza jambo na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Anthony Mihayo.
Viongozi Waandamizi wa Mahakama.
Kikundi cha ngoma Nyota.
Kwaya ya Utumishi wa Umma pamoja na ya Mahakama.
Kwaya ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC), Mhe. Jaji Jacobs Mwambegele.
Bendi ya Polisi.
(Picha na MAGRETH KINABO, INNOCENT KANSHA NA FAUDSTINE KAPAMA- Mahakama, Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni