Na ARAPHA RUSHEKE –Mahakama, Dodoma
Katika kutimiza wajibu wake kisheria, Mahakama ya
Tanzania iliandaa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi Taifa, ambalo linajumuisha
wajumbe kutoka Mahakama mbalimbali za nchini Tanzania.
Baraza hilo ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa PSSSF
Jijini Dodoma kuanzia tarehe 11 na 12 April 2025 liliongozwa na Jaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza
hilo.
Wakiwa katika Baraza hilo, wajumbe walipatiwa elimu
mbalimbali, ikiwemo kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa umma
(PSSSF).
Mada nyingine ilikuwa ni maandalizi ya kustaafu katika
utumishi na uongozi ambayo ilitolewa na Mhadhiri, mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha
Mzumbe Dkt.Venance Shilingi, lakini pia wajumbe hao walipata mada ya afya ya
akili kutoka kwa Bi Sadaka Ahmad Gandi.
Wajumbe walionyesha kufurahishwa na muitikio wa pamoja
kuwa wamefarijika baada ya kuuliza maswali mbalimbali na kupatiwa majibu
sahihi.
Mwenyekiti wa Baraza hilo aliwashukuru watoa mada wote pamoja na wajumbe kwa ushirikiano walioutoa tangu mwanzo mpaka kufikia kikomo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni