Na DOTTO NKAJA-Mahakama, Geita
Hivi karibuni Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Geita, Mhe. Griffin Mwakapeje alifanya ziara
ya ukaguzi wa Mahakama kwenye Kanda hiyo ili kujionea maendeleo ya kiutenda,
kuwaongezea maarifa katika utoaji haki Mahakimu na Watumishi wengine pamoja na
kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.
Mhe. Mwakapeje alifanya
ziara hiyo kwa niaba ya Jaji Mfawidhi, Mhe. Kevin Mhina kwenye Mahakama ya Hakimu
Mkazi Geita, Mahakama ya Wilaya Geita na Mahakama za Mwanzo Nyankumbu, Katoro,
Bugando na Butundwe.
Akiwa katika ziara hiyo, Jaji
Mwakapeje alijionea jinsi Mahakama hizo zinavyokwenda na kasi aliyoelekeza na
Jaji Mfawidhi, ikiwemo kusikiliza mashauri kwa wakati na kwa kufuata misingi
iliyowekwa.
Akizungumuza na Watumishi
katika Mahakama hizo, Mhe. Mwakapeje aliwaasa kujiepukane na vitendo vya rushwa
na kufanya kazi kwa upendo na ushirikiano.
Katika ziara hiyo, Jaji Mwakapeje
aliambatana na Naibu Msajili, Mhe. Fredrick Lukuna, Mtendaji wa Mahakama Geita,
Bi. Masalu Kisasila, Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Mhe.
Clefas Waane, Kaimu Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Geita, Mhe. Bruno Bongole
na Viongozi wengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni