Jumatatu, 16 Juni 2025

MAHAKIMU MBEYA WAPIGWA MSASA UANDISHI WA HUKUMU

Na Daniel Sichula- Mahakama, Mbeya

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga afungua mafunzo ya uendashaji wa Mashauri, uandishi wa hukumu, utoaji wa adhabu na uwekaji wa maamuzi ya Mahakama katika mfumo wa kutunza uamuzi ujulikanao kama TanzLII (Tanzania Legal Information Institute) na matumizi yake katika kufanya utafiti wa kisheria.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi ya mikutano wa Chuo Kikuu cha Catholic Mbeya mnamo tarehe 13 Juni, 2025, yalihudhuriwa na Mahakimu wote wa Mkoa wa Mbeya na Songwe, kuanzia ngazi ya Mahakama ya Mwanzo, Wilaya na Mkoa.

Wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mhe. Tiganga aliwakumbusha Mahakimu hao kuhusu msingi wa suala la maadili na kuwawataka wawapo kwenye mafunzo hayo kuwa huru kujadili kwa namna ya kipekee ili waweze kukiishi kile kitakacho na mafunzo hayo na kukifanyia kazi.

“Suala la maadili linaenda samabamba na utoaji haki kwa hiyo inatupasa kutenda haki kulinga na kiapo cha uhakimu na hili la mafunzo ni njia moja wapo ya kujitambua na kubadili fikra ili tujielekeze katika kutanda haki,” alisema Mhe. Tiganga.

Mhe. Tiganga aliwapongeza washiriki na waandaji wa mafunzo hayo kwani imekua chachu kwa washiriki wote kujifunza na kupata maarifa mapya katika kuendesha shughuli zake.

Vilevile, kuhusu suala la mifumo hasa ule wa TanzLII washirikiri walipitishwa kwenye mfumo huo na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania, Mhe. Kifungo Mrisho alitoa elimu juu ya matumizi ya mfumo huo na kuwakumbusha kupandisha maamuzi ya Mahakama kwa wakati, namna unavyofanaya kazi, matumizi yake na namna mfumo huo unavyoweza kuwasaidia katika kufanya wa tafiti mbalimbali.

Aidha, Mhe. Kalunde pamoja na Mhe. Pomo walitoa elimu kwa washiriki uandishi wa hukumu na undeshaji wa mashauri kwa kufuata sheria na kutenda haki na Mhe. Kishenyi alimaliza kwa kutoa elimu ya utoaji adhabu kwa kufuata sheria na misingi ya utoaji haki.

Aidha, mafunzo hayo yaliyoongozwa jopo la Majaji watatu Mhe. Joachim Tiganga, Mhe. Said Kalunde na Mhe. Musa Pomo pamoja na Naibu Msajili Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Kifungo Kariho Mrisho na sehemu ya Mahakimu waliotoa mafunzo hayo walikuwa Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Songwe Mhe. Francis Kishenyi, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe. Teddy Mlimba.

Viongozi Wakuu wanashiriki mafunzo wakiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mahakimu walioshiriki mafunzo hayo ya uandishi wa hukumu. 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akitoa neno wa kufungua mafunzo hayo.


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Said Kalunde akitoa mada kwa washiriki wa mafunzo ya uandishi wa hukumu.

Naibu Msajili Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Kifungo Kariho Mrisho akitoa mada ya uwekaji wa maamuzi ya Mahakama katika mfumo wa kutunza uamuzi ujulikanao kama TanzLII (Tanzania Legal Information Institute) na matumizi yake katika kufanya utafiti wa kisheria.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni