Ijumaa, 13 Juni 2025

NAIBU MSAJILI SUMBAWANGA ASISITIZA MAADILI NA NIDHAMU KWA WATUMISHI

Na Fredrick Mahava - Mahakama, Sumbawanga.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga Mhe. Joseph Luambano amewataka watumishi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga kudumisha maadili, uadilifu na nidhamu ya hali ya juu kazini.

Mhe. Luambano amesema hayo leo tarehe 12 Juni, 2025 wakati  wa kikao cha watumishi kilichofanyika katika ukumbi  uliopo Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga  alipokuwa anawasilisha salamu za pongezi kwa watumishi kutoka Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma katika ziara iliyofanyika hivi karibuni katika Kanda hiyo.

Baada ya kumaliza ziara, Tume inayo furaha na fahari kubwa kutoa pongezi za dhati kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga, kwa kazi nzuri na yenye kuleta tija katika kutekeleza majukumu ya utoaji haki kwa wananchi. Hivyo naleta rasmi pongezi hizo kwenu watumishi wa Mahakama kwa jinsi ambavyo mliweza kutoa ushirikiano mkubwa kwa wajumbe wa Tume tokea mapokezi mpaka siku ya mwisho waliokuwa wakiondoka katika Kanda yetu hongereni sana,” alisema Mhe. Luambano.

Naye, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Essaba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho alifungua kikao na kutaja agenga za kikao hicho cha watumishi, pamoja na mambo mengine alisisitiza mshikamano miongoni mwa watumishi na kufanya kazi kama timu moja

Vilevile, kikao hicho cha watumishi kilishuhudia baadhi wa watumishi waliohudhuria Mafunzo, Semina na Makongamano mbalimbali katika kipindi kilichopita walipata wasaa wa kuwasilisha taarifa zao. Aidha, Afisa Hesabu Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Bw. Martin Mwandambo aliwasilisha taarifa ya mgao wa fedha ya mwezi Mei, 2025.

Kikao hicho kilihudhuriwa na watumishi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi Rukwa na Mahakama ya Wilaya Sumbawanga.

Naibu Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga akiwasilisha salamu za pongezi kutoka Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Essaba (aliyesimama) akifungua kikao cha watumishi.

Watumishi wa Kada ya Ugavi wakiwasilisha taarifa yao baada ya kuhudhuria Kongamano la wataalam wa Manunuzi na Ugavi

Watumishi wa Mahakama Kada ya Sumbawanga Mwandishi Mwendesha Ofisi wakiwasilisha taarifa yao baada ya kuhudhuria kongamano la Waandishi wwndesha ofisi (TAPSEA)

Watumishi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga wakisikiliza kwa makini wakati wa kikao hicho cha watumishi.

Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni