Marehemu
Michael Christian Kayombo enzi za uhai wake.
TANZIA
Mahakama
ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Michael
Christian Kayombo aliyekuwa akihudumu Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya
Kazi kama Afisa Kumbukumbu Daraja la I.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Divisheni ya Kazi, Bw. Jumanne Muna, marehemu Kayombo alifikwa na
umauti tarehe 13 Juni, 2025 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa
akipatiwa matibabu.
Bw. Muna amesema kuwa, taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika, mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 16 Juni, 2025 katika makaburi ya Kinyerezi-Tabata jijini Dar es Salaam.
Marehemu
Kayombo alizaliwa tarehe 10 Januari, 1992 na aliajiriwa Mahakama ya Tanzania
tarehe 21 Septemba, 2015.
BWANA
AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni