Na INNOCENT KANSHA - Mahakama
Mafanikio
ya maboresho yaliyopatikana ndani ya Mahakama ya Tanzania yanatokana na
ushirikiano madhubuti baina ya Mhimili ya Serikali na Bunge, ushirikiano ambao
unalenga kuimarisha ustawi wa utoaji haki na kujenga misingi imara ya haki kwa
wananchi.
Akitoa
neno fupi la shukurani wakati wa hafla ya Uapisho wa Jaji Mkuu Mpya wa Tanzania
Mhe. George Mcheche Masaju leo tarehe 15 Juni, 2025 katika Viunga vya Ikulu
Chamwino jijini Dodoma, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis
Juma amesema, mashirikiano ya Mihimili hiyo ya Serikali na Bunge yameleta
mapinduzi makubwa ndani ya Mahakama kwani mihimili hiyo ndiyo inayosimamia
rasilimali zinazotumiwa na Mahakama kujenga mifumo imara na kuboresha katika
nyaja ya utoaji haki.
“Watu
wengi wanadhani ule ushirikiano wa mihimili mengine unaingilia uhuru wa
Mahakama siyo kweli, kwa sababu Mahakama inachokitafuta katika ushirikiano ni
rasilimali ya Taifa ambayo inasimamiwa na mihimili mingine. Siku zote ukipata wasaha
wa kukaa na viongozi wa mihimili mingine lazima ujadili mambo yenye maslahi
makubwa kwa ajili ya manufaa ya muhimili wa Mahakama,” ameongeza Jaji Mkuu
Msataafu.
Aidha,
Jaji Mkuu Mstaafu amemshauri Mhe. Masaju kuwa, siku zote afuatilie hotuba za
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwasababu kuna ahadi fulani huwa anazitoa zilizojengeka katika msingi wa utoaji
haki unaweza kuzitumia kama silaha.
“Mimi
nakumbuka tarehe 22 mwezi wa nne mara baada ya kuapishwa kuchukua hatamu ya
kuiongoza nchi alihutubia Bunge la 12 na kuna maneno ambayo aliyasema kuhusu
Mahakama siku zote huwa natembea nayo mfukoni kwa sababu mara zote nikikutana
naye huwa namkubusha juu ya ahadi aliyotoa na ndiyo silaha ambayo Mtendaji Mkuu
akienda hazina uonesha Mhe. Rais aliahidi hivi,” amenukuliwa Jaji Mkuu Mstaafu
huyo.
Akitoa
nukuu ya Mhe. Rais, Mhe. Prof. Juma alisema tutashirikiana pia na Mhimili wa
Mahakama katika kuimarisha mifumo ya utoaji haki, ikiwemo kuendelea kujenga
miundombinu ya Mahakama, kuongeza idadi ya Majaji na Mahakimu na kukuza
matumizi ya TEHAMA ili kuongeza kasi ya usikilizaji wa kesi na uwekaji wa
kumbukumbu.
Jaji
Mkuu Mstaafu ameongeza kuwa, Mhe. Rais anaweza kuwa na shahuku ya kuiimarisha
mfumo wa utoaji kwani anajua kuwa, maendeleo yoyote ya kiuchumi hayawezekani
bila ya kuwa na Mahakama huru, bila kuwa na utawala wa sheria. Hivyo Mhe. Rais
ni mdau muhimu sana na ndiyo maana ukiangalia programu za maboresho zinajaribu
kujiengesha kwenye dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 kwa sababu dira hiyo
ina ahadi ya rasilimali ambazo Mpango Mkakati wa Mahakama ulijiengesha huko ili
kunafaika na rasilimali hizo.
Vilevile,
Mhe. Prof. Juma ameongeza kuwa, Mhe. Rais anatambua kuwa, utoaji wa haki ni
sehemu muhimu sana ya maendeleo ya nchi, kwamba ukiwa na Mahakama imara
inayofuata sheria na taratibu inaleta utulivu ambao unahitajika katika
shughuliza za kujenga uchumi ulioimara na kustawisha Taifa.
Sheria
ya Usimamizi wa Mahakama sheria namba nne (4) imesaidia sana kwani imeimarisha
uhuru wa Mahakama kwani Serikali na Bunge ndiyo vyombo vinavyosimamia
rasilimali, sasa basi Mahakama inazifikia hizo rasilimali kupitia Mtendaji Mkuu
wa Mahakama na Msajili Mkuu wa Mahakama kwa sababu mara nyingi Jaji au Msajili
akionekana anazunguka zunguka Hazina watu wengine wanadhani uhuru wa Mahakama
upo mashakani.
Jaji
Mkuu Mstaafu Mhe. Prof. Juma ameongeza kuwa, lakini akionekana Mtendaji Mkuu wa
Mahakama akizunguka hazina na kufanikisha yote aliyokuwa anatafuta utaweza
kuona kwamba hiyo sheria ya usimamizi wa Mahakama ni msingi imara sana ambao
umeiwezesha Mahakama kuwa huru zaidi, na vilevile kuweza kupata rasilimali
kutoka mfuko mkubwa wa Serikali
“Nakushuru
sana Mhe. Rais pamoja na kunipa mazingira ya kufanya kazi kwa utulivu ila
uwezeshaji ulikuwa ni mkubwa sana, uwezeshaji ambao ulileta utulivu na utivu wa
kipekee katika Mahakama na hilo ni somo ambalo nitamuomba Jaji Mkuu Mpya Mhe.
George Mcheche Masaju kwamba usiache kuangalia jicho la Mhe. Rais kwasababu
yeye ni mdau mwezeshaji,” amesema Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Prof. Juma.
Mhe.
Prof. Juma ameongeza kuwa, maboresho yote yaliyopatikana na kuyaona siyo nguvu
ya Prof. Juma ya uwezeshaji ama nguvu ya Majaji, ni nguvu ya uwezeshaji kutoka
Serikali Kuu chini ya Mhe. Dkt. Samia ambaye amekuwa mara zote akitaka Mahakama
kutatua kero za wananchi kupitia Mahakama.
“Nakuhakikishia
kwamba, Uongozi mzima wa Mahakama tulikaa tukajadiliana tukasema kwamba
tutakupa utiifu, unyenyekevu wa hali ya juu ili kukuwezesha wewe utuongoze ili
tuweze kufikia malengo ya utoaji wa haki kwa sababu haya malengo ni endelevu
viongozi wote wa Mahakama waliopo mbele yako ni viungo na wako tayari kukupa
ushirikiano ukiwa na jambo lolote ambalo ni la nje ya mhimili hawa viungo
watakupa ushirikiano mkubwa kulitatua,” ameongeza Mhe. Prof. Juma.
Aidha,
Mhe. Prof. Juma akatoa rai kwa Jaji Mkuu mpya Mhe. Masaju kwamba, jicho lake
lazima likamate jicho la Mhe. Rais kwa kuangalia anafanya nini na je hicho
anachokifanya kitasaidiaje Mahakama kwa sababu Mhe. Rais ni mdau muhimu sana
bila uwekezaji wake hakuna chochote Mahakama inaweza kukifanya, kweni ndiye
anayeongeza Majaji, Mahakimu, rasilimali fedha za miundombinu na watumishi
waoisaidia Mahakama kutenda haki.
Aidha,
Itakumbukwa kuwa Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa sita (6) Mzalendo mnamo mwaka 2017 na
aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli na kuhudumu katika cheo hicho kuanzia 2017 hadi 2025.
Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa nasaa zake wakati wa hafla ya kumwapisha Jaji Mkuu mpya wa Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju leo Tarehe 15 Juni, 2025 Ikulu Chamwino jijini Dodoma
Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye hafla ya uapisho wa Jaji Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju Ikulu Chamwino jijini Dodoma akiwa wakati wa uapisho huo.
Sehemu ya Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa kwenye hafla ya kumwapisha Jaji Mkuu wa Tanzania mpya Mhe. George Mcheche Masaju wakiwa Ikulu Chamwino jijini Dodoma akiwa wakati wa uapisho huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na familia ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju mara baada ya kuapishwa kwake Ikulu Chamwino jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Mahakama ya Tanzania mara baada ya kuwasili kwenye chumba maalumu cha kupumzikia wageni alipowasili kwenye jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma mara baada ya uapisho wake wa kushika wadhiwa wa Jaji Mkuu wa Tanzania.
(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni