Jumatatu, 14 Julai 2025

TANZIA; AFISA HESABU MWANDAMIZI MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KATAVI AFARIKI DUNIA

Marehemu Jociah Daniel Malongo enzi za uhai wake.

 TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Afisa Hesabu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi, Bw. Jociah Daniel Malongo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Julai, 2025 na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi, Bw. Epaphras Tenganamba marehemu Malongo alifikwa na umauti Siku ya Jumamosi tarehe 12 Julai, 2025 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Bw. Tenganamba amesema kuwa, taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika na marehemu Malongo anatarajiwa kuzikwa Siku ya Alhamis tarehe 17 Julai, 2025 katika Kijiji cha Ukingwaminzi Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu. 

Marehemu Malongo alizaliwa tarehe 04 Aprili, 1975 na aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania tarehe 20 Juni, 2005 kama Msaidizi wa Hesabu. Marehemu ameacha mjane na watoto wanne.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba huo mzito wa kuondokewa na Mpendwa wetu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni