Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro leo tarehe 11 Julai 2025 ametembelea Banda la
Mahakama katika maonesho ya 49 ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba), 2025 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Temeke Dar es Salaam.
Mhe.
Dkt. Ndumbaro akiwa kwenye mabanda hayo alijionea watumishi wa Mahakama wanaotoa
elimu kwa Wananchi mbalimbali wanaofika kupewa elimu
hiyo ya kisheria na taratibu mbalimbali za uendeshaji wa shughuli za
kimahakama.
“Mimi nimekuwa mdau na mpiga debe wa maboresho ya shughuli za
Mahakama kwa mda mrefu na nitaendelea kufanya hivyo kwani Mahakama ni chombo
chetu sote, vilevile niwapongeze kwa kazi kubwa mnayofanya ya kutoa elimu kwa
umma hili ni jambo jema sana,” amesema Mhe. Dkt. Ndumbaro
Itakumbukwa kwamba, maonesho hayo yatahitimishwa tarehe 13 Julai, 2025
na Waziri huyo akatoa rai kwa wananchi mbalimbali kuendelea kutembelea
Banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba), 2025 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Temeke Dar es Salaam.
(PICHA NA INNOCENT KANSHA - Mahakama 77)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni