Na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania leo tarehe 17 Oktoba, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Viongozi hao kutoka CMA wamepatiwa ushauri na maoni mbalimbali kutoka kwa Viongozi wa Mahakama yote yakilenga kuboresha huduma za utatuzi wa migogoro ya kazi zinazotolewa na Tume hiyo pamoja na kuboresha ushirikiano kati ya Tume na Mahakama.
Viongozi wa Mahakama walioshiriki katika mazungumzo hayo ni pamoja na Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdi Kagomba, Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Herbert, Makatibu Binafsi wa Jaji Mkuu, Mhe. Venance Mlingi na Mhe. Clarence Mhoja
Matukio katika picha mazungumzo kati ya Mahakama na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi mbele) akiwa kwenye kikao na Viongozi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akizungumza jambo wakati wa kikao na Viongozi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Herbert (kushoto) akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mahakama na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdi Kagomba.
Katibu Binasfi wa Jaji Mkuu, Mhe. Clarence Mhoja akiwa katika kikao kati ya Mahakama na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni