Ijumaa, 17 Oktoba 2025

JAJI MKUU AMUAPISHA HAKIMU MKAZI MPYA

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 17 Oktoba, 2025 amemuapisha Mhe. Hillary Massala Kuzenza kuwa Hakimu Mkazi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Mhe. Masaju amemtaka Hakimu huyo kurejea hotuba yake aliyoitoa tarehe 07 Oktoba, 2025 alipowaapisha Mahakimu wenzake wapya.

Uapisho huo umehudhuriwa na Viongozi kadhaa wa Mahakama wakiwemo Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdi Kagomba, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, Kaimu Msajili Mkuu ambaye ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Herbert George, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Chiganga Tengwa.

Wengine ni Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Emmanuel Mrangu, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Kuu, Mhe. Mwajabu Mvungi, Watendaji wa Mahakama Kuu Masjala Kuu, Bw. Humphrey Paya na Bw. Ginaweda Nashon, Mkurugenzi wa Mafunzo ya Kimahakama kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Dkt. Patricia Kisinda, Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu na wengine.

Matukio katika picha ya Uapisho wa Hakimu Mkazi, Mhe. Hillary Massala Kuzenza.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akimuapisha Mhe. Hillary Massala Kuzenza kuwa Hakimu Mkazi leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.


Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdi Kagomba (kulia) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante wakiwa katika hafla ya uapisho wa Hakimu Mkazi  mpya iliyofanyika leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Sehemu ya Viongozi na watumishi wa Mahakama waliohudhuria katika Hafla ya Uapisho wa Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Hillary Massala Kuzenza leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.


Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akisaini hati ya kiapo cha Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Hillary Massala Kuzenza mara baada ya kumuapisha leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.


Hakimu Mkazi, Mhe. Hillary Massala Kuzenza  (kushoto) akisaini hati ya kiapo mara baada ya kula kiapo cha kushika wadhifa huo mbele ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia). Aliyesimama katikati ni Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Herbert.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akizungumza jambo mara baada ya kumuapisha Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Hillary Massala Kuzenza (hayupo katika picha) leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.


Hakimu Mkazi aliyeapishwa leo tarehe 17 Oktoba, 2025, Mhe. Hillary Massala Kuzenza akisikiliza kwa makini mawaidha yaliyokuwa yakitolewa na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuapishwa kwake.


Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kushoto) akizungumza na Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Hillary Massala Kuzenza (aliyesimama kulia) mara baada ya kumuapisha kushika wadhifa huo leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdi Kagomba akizungumza jambo wakati wa hafla ya uapisho wa Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Hillary Massala (hayupo katika picha).

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa neno wakati wa hafla ya Uapisho wa Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Hillary Massala Kuzenza (hayupo katika picha).


Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akimpongeza Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Hillary Massala Kuzenza mara baada ya kumuapisha kushika wadhifa huo leo tarehe 17 Oktoba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdi Kagomba (kushoto) na Hakimu Mkazi mpya aliyemuapisha leo, Mhe. Hillary Massala Kuzenza (kulia).



Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) pamoja na baadhi ya Viongozi wengine wa Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Hillary Massala Kuzenza (wa tatu kulia). Wa tatu kushoto ni Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdi Kagomba (wa tatu kushoto), wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, wa pili kushoto ni Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Herbert, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu.

(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)









Hakuna maoni:

Chapisha Maoni