Na ARAPHA RUSHEKE, Mahakama – Dodoma.
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma,
hivi karibuni ilifanya kikao na wadau ili kutathmini utendaji kazi wa mwaka
2025 na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za utoaji haki kwa mwaka 2026.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma, kilifunguliwa na Jaji
Mfawidhi, Mhe. Dkt. Juliana Masabo. Mhe. Dkt. Masabo alieleza kuwa kikao hicho
ni sehemu ya utamaduni wa Mahakama kukutana na wadau wake ili kufanya tathmini
ya pamoja na kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma.
Mhe. Dkt. Masabo alieleza kuwa lengo lingine
ni kuangalia kwa pamoja utendaji kazi wa mwaka uliopita, kubaini mafanikio na
changamoto zilizojitokeza, na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha maeneo
yaliyohitaji uboreshaji.
Alisisitiza kuwa Mahakama Kuu Kanda ya
Dodoma, inayojumuisha Mikoa ya Dodoma na Singida, ina wajibu mkubwa kutokana na
Dodoma kuwa Makao Makuu yaNnchi, hivyo mabadiliko yanayoendelea yanahitaji kasi
na ubora zaidi katika utoaji haki.
Aidha, alibainisha lengo jingine ni
kuimarisha ushirikiano kati ya Mahakama na wadau, ambao ni nguzo muhimu katika
utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama. Kupitia vikao vya namna hiyo, wadau
wamekuwa wakipanga pamoja na kutekeleza majukumu kwa pamoja, jambo
lililochangia kuongeza ufanisi wa utendaji.
Akizungumzia mafanikio ya mwaka uliopita wa
2025, Mhe. Dkt. Masabo alisema Mahakama ilipokea mashauri zaidi ya 1,000 na pia
kufanikiwa kumaliza mashauri zaidi ya 1,000. Alibainisha kuwa mafanikio hayo
yametokana kwa kiasi kikubwa na ushirikiano wa wadau mbalimbali, wakiwemo Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mawakili wa Kujitegemea, Mabaraza ya Ardhi,
Ofisi ya Kamishna wa Ardhi, Msajili wa Hati, pamoja na Taasisi nyingine
zinazohusika na masuala ya kisheria na kiutawala.
Aliongeza kuwa mashauri mengi yaliyopokelewa
na kumalizwa yalihusu masuala ya ardhi, jambo linaloonesha umuhimu wa
ushirikiano wa karibu na taasisi zinazohusika na sekta hiyo.
Katika kikao hicho, wadau walipata pia fursa
ya kujifunza mambo mbalimbali zitakazowasaidia katika utekelezaji wa majukumu
yao ya kila siku.
Akisoma taarifa ya mashauri katika kikao hicho, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe Silivia Lushasi, alibainisha mikakati mbalimbali ya kuzuia mashauri kukaa muda mrefu mahakamani kwa mwaka 2026.
Meza kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Masabo [aliyepo katikati] ikiwa inasikiliza kwa makini maoni na ushauri kutoka kwa wadau waliodhuria kikao hicho, aliyepo kulia kwake ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Amir Mruma na aliyepo kushoto kwake ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Silvia Lushasi.
Washiriki
wa kikao wakiogozwa na Jaji Mfawdhi (hayupo pichani) wakisikiliza kwa makini
wasilisho kutoka kwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Dodoma, Mhe. Silivia Lushasi
(hayupo pichani).
Meza
kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana
Masabo [aliyepo katikati] ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu
Dodoma pamoja Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali waliohudhuria kikao hicho, walioketi
kulia kwake ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Amir Mruma na aliyepo
kushoto kwake ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Silvia
Lushasi.
Meza
kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana
Masabo [aliyepo katikati] ikiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu pamoja na
wadau kutoka Taasisi mbalimbali waliohudhuria kikao hicho.
Meza
kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana
Masabo [aliyepo katikati] ikiwa katika picha ya pamoja na Si.ekretariet





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni