Alhamisi, 5 Februari 2026

WATUMISHI WA MAHAKAMA KUU MUSOMA WATEMBELEA WATOTO WENYE MAHITAJI

Na FRANCISCA SWAI-Mahakama, Musoma

Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, jana tarehe 04 Februari 2026, walitembelea Kituo cha Watoto wenye mahitaji maalum na kutoa msaada wa vitu mbalimbali muhimu.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya, aliwaongoza watumishi hao, ambao walitembelea Kituo cha Al-Jaziira Orphan Centre kilichopo Kijiji cha Mkirira, Kata ya Nyegina, Musoma Vijiji. Kituo hicho kinahudumia watoto wa kiume wenye umri wa miaka minne hadi 15.

Akitoa shukrani kwa watumishi wa Mahakama, Kaimu Meneja wa Kituo hicho, Bw. Said Masaka, alisema Kituo hicho kina mahitaji mengi, ikiwa ni pamoja na elimu ya ushauri wa kisheria kuhusu haki za motto, mafunzo ya sheria ya mtoto kwa walezi na watumishi, pamoja na msaada wa kusimamia sera ya ulinzi wa mtoto.

Ombi hilo lilipokelewa na uongozi wa Mahakama ambapo waliahidi kwenda kujipanga ili kuwapa elimu hiyo hivi karibuni.

Aidha, pamoja na tendo jema hilo, watumishi wa Mahakama walipata pia elimu kuhusiana na masuala ya kibenki na fedha kutoka kwa watumishi wa Benki ya NMB Musoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Tendo Jema, Bw. Musa Komba, akimkabidhi Kaimu Meneja wa Kituo cha Al-Jaziira Orphan Centre, Bw. Said Masaka, zawadi mbalimbali kutoka kwa watumishi wa Mahakama Musoma.

Watoto wa kituo cha Al-Jaziira Orphan Centre (waliosimama katikati) wakiongoza dua ya kuwashukuru na kuwaombea watumishi na Mahakama ya Tanzania.

Kaimu Meneja wa Kituo cha Al-Jaziira Orphan Centre, Bw. Said Masaka [wa kwanza kushoto] akisikiliza kwa makini salamu za Mahakama zinazotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Tendo Jema, Bw. Musa Komba, [aliyesimama katikati].

Picha ya pamoja ya watumishi wa Mahakama Musoma, viongozi na walimu wa kituo cha Al-Jaziira Orphan Centre.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akiwa pamoja na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Monica Ndyekobora (wa pili kushoto) pamoja na watumishi wa Benki ya NMB waliotoa elimu ya masuala ya kifedha kwa watumishi wa Mahakama Musoma.

 Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Morogoro.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni