· Jaji Mfawidhi asisitiza mwisho wa matumizi ya karatasi katika uendeshaji wa mashauri
Na NAUMI SHEKILINDI, Mahakama-Simiyu
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Simiyu, Mhe Wilbert Chuma
amewaongoza watumishi wa Kanda hiyo na WanaSimiyu katika kuadhimisha Siku ya Sheria
nchini 2026.
Mhe.
Chuma ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya
Sheria mkoani humo aliambatana na Mgeni Maalum Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anamringi Macha KATIKA sherehe hizo zilizofanyika tarehe 02 Februari, 2026 katika
viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Simiyu.
Akizungumzia
kuhusu Kauli Mbiu ya Siku ya sheria nchini, 2026 isemayo; ‘Mchango wa Mahakama katika ustawi na maendeleo ya Taifa’ Jaji
Mfawidhi alisema kuwa, Kauli Mbiu hiyo ina dhamira ya kutambulisha kwa umma
nafasi ya Mahakama katika kuleta maendeleo na ustawi wa Taifa na kudhihirisha
kuwa haki na maendeleo havitengani.
Mhe.
Chuma alisisitiza kuwa, haki inapopatikana kwa wananchi kwa uwazi na kwa
kufuata misingi ya sheria hujenga imani kwa Taasisi za Haki na kuweka mazingira
bora ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Aidha,
Mhe. Chuma alizungumzia juu ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) ili kuepukana na matumizi ya karatasi na kusema kuwa, “huduma za Mahakama
kwa njia ya mtandao zimeimarishwa, hatua iliyosaidia kusogeza haki karibu zaidi
na wananchi bila gharama kubwa za usafiri.”
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anamringi Macha alisisitiza watumishi
wa Mahakama kuwa na uadilifu, weledi na uwajibikaji ili kuweza kutoa haki kwa
wananchi.
Naye
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Simiyu, Mhe. Elimo Massawe aliongoza
wadau kwa ajili ya kwenda kusikiliza shauri la jinai la kwanza kusikilizwa
katika Mahakama Kuu Kanda ya Simiyu.
Hotuba
nyingine zilitolewa na Viongozi kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka na Ofisi ya
Mawakili wa Kujitegemea wote wakisisitiza kwamba Mahakama ndio nguzo ya
maendeleo na maendeleo ndio azma ya Serikali ili kuleta ustawi na haki kwa
jamii, vilevile walieleza kuwa, ustawi wa maendeleo ni matokeo ya Mihimili yote
mitatu yaani Mahakama, Serikali Kuu na Bunge.
Maadhimisho
hayo yalihudhuriwa na watumishi pamoja na wadau kutoka Taasisi mbalimbali
wakiwemo Wadau kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka, Mawakili wa Kujitegemea,Taasisi
ya Kuzui ana Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), PSSSF, NHIF, TRA, Polisi, Uhamiaji
na wananchi kwa ujumla.
Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Simiyu, Mhe. Wilbert Chuma (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama Kuu Simiyu. Wa pili kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Simiyu, Mhe. Elimo Massawe, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kainunula, wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anamringi Macha pamoja na wa kwanza kushoto ni Wakili wa Kujitegemea, Wakili Sabini.
(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni