Na. MUKSINI NAKUVAMBA - Mahakama Mbeya
Watumishi
wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya wamepata elimu muhimu ya afya ya kinywa na meno
tarehe 9 Februari, 2026. Elimu hiyo ilitolewa na Daktari Melkzedeck Japhet
kutoka kliniki ya Confort Dental Care iliyopo Mwanjelwa, Jijini Mbeya.
Akitoa
elimu hiyo Daktari Japhet alisisitiza mambo muhimu yakuzingatia ikiwemo, usafi
wa kinywa ambapo Daktari alisisitiza kuhusu kusafisha meno angalau mara mbili
kwa siku hasa usiku kabla ya kulala, kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari
nyingi ili kuzuia kuoza kwa meno na afya ya fizi ambapo daktari alisema dalili
za magonjwa ya fizi, namna ya kuyatambua na matibabu yake.
Aidha
Daktari Japhet aliongezea kwa kuwaasa watumishi hao kuvunja dhana potofu
kuhusiana na magonjwa ya meno na matibabu ya meno kwa mama mjamzito na kueleza
kuwa Mama mjamzito anaweza kupata matibabu ya meno inapohitajika, hakuna “mdudu
mtoboa jino” bali ni bakteria na asidi zinazotokana na sukari na kwamba kung’oa
jino si lazima kufanyika asubuhi pekee na chakula kinaweza kuliwa kabla ya
kung’oa jino kulingana na ushauri wa daktari, mambo ambayo walio wengi huwa na dhana
potofu.
Kwa
upande wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim
Tiganga, alitoa shukrani kwa daktari kwa kutenga muda na kutoa elimu hiyo, alisisitiza
kuwa elimu hiyo imewafanya watumishi wa mahakama kutambua zaidi umuhimu wa
kujali afya ya kinywa na meno kwa maisha bora na ufanisi kazini.
Daktari
Melkzedeck Japhet (aliyesimama) akitoa elimu ya Afya ya kinywa na meno
mbele ya watumishi wa Mahakama kuu Mbeya.
Afisa Utumishi kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Bi. Sarah Rossi (wa pili kushoto)
akiuliza swali kwenda kwa mtaalamu wa afya wakati wa utoaji elimu ya afya ya
kinywa na meno.
Naibu
Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu (wa pili kulia)
akiuliza swali Kwenda kwa mtaalamu wa afya wakati wa utoaji elimu ya afya ya
kinywa na meno.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Tiganga (wa kwanza
Kulia), Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu
(Katikati), na wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi.
Mervis Miti wakipata elimu ya afya ya kinywa na meno.
Sehemu
ya watumishi wa Mahakama Kuu Mbeya wakipata elimu kutoka kwa Mtaalamu wa Afya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni