Na. MUKSINI NAKUVAMBA- Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Tiganga, ameongoza viongozi
na watumishi wa Mahakama katika hafla maalum ya kumtakia kheri na baraka, Jaji
wa Mahakama Kuu Mhe. Victoria Mlonganile Nongwa kufuatia uteuzi wake wa kuwa
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Njombe.
Hafla
hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, ilihudhuriwa
na Viongozi na Watumishi mbalimbali wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Njombe,
Songwe na Iringa. Vilevile watumishi walipata wasaa wa kutoa shukrani, pongezi
na kumbukumbu za namna Mhe. Nongwa alivyogusa maisha ya wengi kupitia uongozi
wake.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim
Tiganga alimpongeza Mhe. Nongwa kwa utendaji wake uliotukuka na uwezo wake wa
kujenga mshikamano miongoni mwa watumishi, akibainisha kuwa ameacha alama isiyofutika
katika utumishi wa Mahakama hiyo.
“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuteuliwa kwako
kuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Njombe, tumeshuhudia
uongozi wenye busara, upendo na ushirikiano kutoka kwako. Umeweza kuunganisha
watumishi na kujenga mazingira ya kazi yenye kuheshimiana na kusaidiana,”
alisema Mhe. Tiganga.
Naye,
Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu alisema, Uongozi
bora wa Mhe. Nongwa ulipekea kutunukiwa tuzo mbalimbali za uchapakazi bora kwa
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.
“Umekuwa kiongozi na mshauri mzuri katika
kutekeleza majukumu ya utumishi wako hapa Mbeya, umekuwa na utayari wa kipekee
sana mpaka kutunukiwa tuzo mapema Februari 2026 na Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya
kwa kutambua na kuthamini utayari wako wakati wote katika kutekeleza majukumu
ya kimahakama hata pale uliposhtukizwa wewe ulikuwa tayari kupokea majukumu
hayo ya usikilizaji wa mashauri ambalo ni jukumu mama la Mahakama ya Tanzania,”
alisema Naibu Msajili huyo.
Kwa
upande wake, Jaji Mfawidhi mteule wa Mahakama Kuu Kanda ya Njombe Mhe. Victoria
Nongwa alitoa shukrani kwa watumishi wenzake kwa ushirikiano waliompatia katika
kipindi chote cha utumishi wake katika Kanda ya Mbeya, akieleza kuwa mafanikio
aliyoyapata yametokana na mshikamano na moyo wa pamoja kazini.
“Naondoka nikiwa na kumbukumbu nzuri ya kufanya
kazi na timu yenye upendo na mshikamano. Nitaendelea kuthamini mahusiano haya
hata ninapoanza majukumu yangu mapya mkoani Njombe na nayabeba mazuri yote ya
Mbeya,” alisema Mhe. Nongwa.
Sehemu
ya watumishi waliohudhuria hafla hiyo walieleza kuwa, Mhe. Nongwa alikuwa
kiongozi aliyesikiliza, aliyejali ustawi wa watumishi na aliyehamasisha
utendaji kazi wa pamoja, hali iliyochangia kuongeza ufanisi katika utoaji wa
huduma za haki.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (aliyesimama) akitoa
nasaa zake kwa Viongozi na watumishi wa Mahakama (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Njombe Mhe. Victoria Nongwa (aliyesimama) akizungumza machache na Viongozi na Watumishi wa Mahakama katika hafla ya kuagwa kwake.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo (aliyesimama) akitoa neno la shukurani katika hafla hiyo.
Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Bi. Marvis Miti (aliyesimama) akitoa neno la shukurani katika hafla hiyo
Sehemu ya watumishi waliohudhuria katika hafla hiyo.
Sehemu ya watumishi waliohudhuria katika hafla hiyo.
Sehemu ya watumishi waliohudhuria katika hafla hiyo.
Viongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na Njombe
wakiwa wameshikana mikono kwa pamoja ikiwa ni ishara ya upendo na mshikamano.
Sehemu ya watumishi waliohudhuria katika hafla hiyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbeya Mhe.
Tedy Mlimba (aliyesimama) akitoa shukurani kwa niaba ya Mahakimu wa Kanda ya
Mbeya na Songwe waliohudhuria katika hafla hiyo.
Mmoja wa watumishi (aliyesimama) akitoa neno la
shukurani kwa niaba ya watumishi wengine katika hafla hiyo.
Viongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na Njombe
wakiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watumishi waliohudhuria katika hafla
hiyo mbele ya Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya mbeya.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni