Na. LORDGARD KILALA-Mahakama, IJC Temeke
Maderev
awa Mahakama kutoka Divisheni za Mahakama Kuu ya Tanzania, hivi karibuni walipatiwa mafunzo maalum kwa
lengo la kuboresha utendaji kazi
na utoaji huduma zenye tija na ufanisi zaidi.
Akizungumza katika
ufunguzi wa mafunzo
hayo, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kituo
Jumuishi cha Masuala ya Familia
Temeke, Bw. Samson Mashalla, alisema
kuwa,
Mahakama ya Tanzania katika kutekeleza
jukumu lake la msingi la utoaji
haki kwa wote na kwa wakati, haiwezi kuiacha nyuma kada muhimu ya Madereva.
“Ndio
maana mafunzo haya yameandaliwa kwa nia ya kuwajengea uwezo katika kutekeleza
majukumu yenu
ipasavyo, kwa
kuzingatia baadhi yanu mmeajiriwa hivi karibuni,” alisema Bw. Mashalla aliyefunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa - IJC
Temeke kwa niaba ya Mtendaji wa Mahakama Kuu
Divisheni.
Bw.
Mashalla aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia yote
yatakayofundishwa na mwezeshaji na kuhakikisha wanaenda kuyafanyia kazi kwa
lengo la kuleta tija kwa Taasisi na Serikali kwa ujumla.
Mwezeshaji kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Bw. Ally Kilimila aliwapitisha
washiriki katika mada nne; Maadili
katika utumishi wa Umma, Utunzaji wa Magari ya Serikali, Udereva wa kujihami na
Ukagauzi wa Magari.
Akasisitiza kwamba
nidhamu kwa Dereva ni taswira katika utendaji wake ambayo inahusisha utii wa
dhati wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma kwa kuwa nadhifu, tabia njema,
utunzaji wa siri na muda, nidhamu ya dhati badala ya nidhamu ya woga.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni