Bi. Lightness Elia Kiula wakati wa uhai wake.
Mahakama ya Hakimu Mkazi
Dar es Salaam Kisutu inasikitika kutangaza kifo cha Ofisa Tawala Mwandamizi, Bi.
Lightness Elia Kiula, aliyekuwa akihudumu katika Mahakama ya Wilaya Kigamboni.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bi. Athanasia Kabuyanja, kifo hicho kimetokea tarehe
04 Machi, 2026 katika Hospitali ya Moyo ya Jakaya (JKCI) iliyopo Upanga Dar es
Salaam.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa,
Jina Lake lihimidiwe. Amen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni