Na. Sharifu Mokiwa - Mahakama, Sumbawanga
Watumishi
wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga wamepata mafunzo maalumu
kuhusu mafao na maandalizi ya kuustaafu ambayo yalitolewa kwa njia mbili yaani uso
kwa uso kwa waliokuwepo ukumbini na kwa njia ya Mtandao kwa waliokuwa mbali.
Mafunzo
hayo yalifanyika tarehe 6 Machi 2026, katika ukumbi wa Mahakama Kuu Sumbawanga na yalifunguliwa na Mtendaji wa
Mahakama Kuu Sumbawanga Bw. Machumu Essaba, kabla ya kuanza kuwasilishwa
kwa mada na Afisa kutoka Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi (PSSF) Bw. Eribariki Nsulau
Akizungumza
wakati wa kuwasilisha mada Bw. Nsulau alitoa elimu kuhusu huduma na mafao
yanayo tolewa na PSS, alifafanua jinsi ya kujisajili kwenye portal ya PSSF kuangalia
michango, kuandikisha michango mipya, nakupata mafao mbalimbali, mafao hayo ni
pamoja na fao la mishahara miwili endapo mfanyakazi atapoteza ajira ,fao la uzazi
ndani ya siku 90 na malipo ya pensheni kuanzia tarehe 21- 23 au 21-25 ya mwezi,
yanayolipwa pia kwa wategemezi wa mstaafu. Mafunzo hayo pia yalisisitiza umuhimu
wa uhakiki wa kila mwaka kwa wastaafu na wategemezi ili malipo ya pensheni
yaendelee bila usumbufu.
Kwa
upande wake, Jaji wa Mahakama Kuu Sumbawanga, Mhe. Abubakari Mrisha alitoa
mwongozo wa kitaalamu kuhusu maandalizi ya kustaafu na alisisitiza kuwa
maandalizi ya kustaafu yanapaswa kuanza mapema mara tu mtumishi anapopata cheki
namba, kwani namba hiyo inaonesha muda unaotarajiwa wa kustaafu.
Alieleza
kuwa ni muhimu kwa watumishi kupanga maisha yao ya baadae mapema ili kuepuka changamoto pindi wanapo
staafu.
Aidha,
watumishi walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu mafao, pensheni, mirathi,
na namna ya kujiandaa kustaafu ambapo, mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza
uelewa na uwajibikaji wa watumishi katika kupanga mustakabali wao wa kifedha, huku
wakiongezwa ujuzi muhimu kuhusu hifadhi ya jamii na usimamizi wa michango.
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda, Sumbawanga Bw. Machumu Essaba akifungua rasmi mafunzo kuhusu mafao na maandalizi ya kustaafu kwa watumishi wa Mahakama tarehe 6 Machi, 2026.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda, Sumbawanga Mhe. Abubakari
Mrisha (aliyenyanyua mkono) akisisitiza umuhimu wa maandalizi mapema ya kustaafu kwa watumishi wa
Mahakama Sumbawanga.
Hakimu Mkazi Mhe. Willington Rwabinyasi
akiuliza swali kuhusu mafao na maandalizi ya kustaafu wakati wa mafunzo.
Watumishi wa Mahakama Kuu Sumbawanga
wakisikiliza mafunzo kuhusu mafao na maandalizi ya kustaafu.
Afisa kutoka PSSF Bw. Elibariki Nsulau akipokea
maswali kwa kuyaandika kutoka kwa watumishi wa Mahakama ya Sumbawanga kuhusu
mafao na maandalizi ya kustaafu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni