Na DOTTO NKAJA – Mahakama Kuu, Geita
Wanawake wa Mahakama Kanda ya Geita kutoka Mahakama
Kuu Geita, Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Mahakama ya Wilaya ya Geita na
Mahakama ya Mwanzo Nyankumbu, tarehe 28 Machi
2026 walitembelea Wodi ya Wajawazito na Wazazi katika Kituo cha Afya
Kasamwa.
Lengo la ziara hiyo ni kufanya matendo ya huruma ikiwa
ni utaratibu waliojiwekea kila mwaka wanapoadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake
Duniani.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa
Kituo cha Afya Kasamwa, Dkt. Emmanuel Zillagera, pamoja na Watumishi wengine wa
Kituo hicho waliwaongoza Wanawake wa Mahakama katika wodi hizo na kutoa zawadi
mbalimbali.
Watumishi hao wa Mahakama
walitoa vifaa na mahitaji kwa Wajawazito na Wazazi ambavyo ni sukari, sabuni za
unga, mafuta ya kujipaka, pampers na vingine.
Akizungumza mara baada ya
kupokea msaada huo, Dkt. Zillagera aliwashukuru Wanawake wa Mahakama kwa
matendo ya huruma waliyotoa. Pia aliwaomba kurudi kipindi kingine kwa ajili ya hiyo
mara watakapopata nafasi.
Naye Mtendaji wa Mahakama
ya Tanzania Kanda ya Geita, Bi. Masalu Kisasila, aliwashukuru Viongozi pamoja
na Watumishi wa Kituo hicho kwa kuwakubalia kufika na kufanya matendo ya
huruma.
"Kila mwaka Wanawake wa Kanda ya Geita wanapokuwa wanaelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, hufanya matendo ya huruma kwa kupeleka vifaa ambavyo ni mahitaji mbalimbali. Kitendo hiki ni sadaka yetu kama Wanawake kwa Wazazi pamoja na Wajawazito,” alisema.
Mtendaji wa Mahakama ya
Tanzania, Bi. Masalu Kisasila, akikabidhi sabuni, pampers na vitu vingine kwa Muuguzi
Mkunga Sr. Joyce wa Kituo cha Afya Kasamwa.
Watumishi wa Mahakama Kanda
ya Geita wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufika katika Kituo cha Afya Kasamwa.
Watumishi wa Mahakama
Kanda ya Geita wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Kituo cha Afya
Kasamwa (juu na chini).
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni