Na MUKSINI NAKUVAMBA - Mahakama Mbeya.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga
amewataka Mahakimu pamoja na watumishi wengine wa Mahakama kufanya kazi kwa
kuzingatia maadili na taratibu za utumishi wa umma.
Ameyasema
hayo hivi karibuni wakati akifanya ukaguzi wa Mahakama Mkoa wa Songwe pamoja na
Wilaya ya Mbarali unaolenga kukumbushana kuhusu majukumu ya kila siku na kubaini
mapungufu, changamoto na kuona mapendekezo na njia sahihi za kutatua changamoto
hizo.
“Fanyeni
kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na nidhamu kama njia ya
kuelekea kuhitimisha utumishi katika hali inayofaa” alisema Mhe. Tiganga
Mhe.
Tiganga aliwasisitiza watumishi hao kuongeza kasi katika umalizaji wa mashauri
kwa kuzingatia lengo mama la Mahakama ya Tanzania ambalo ni kusikiliza mashauri
na kuyatolea maamuzi mapema ipasavyo. Vilevile Mhe. Tiganga aliwaasa watumishi kuendelea
kudumisha ushirikiano mzuri uliopo eneo la kazi.
Kwa
upande wake, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi. Mavis Francis Miti, alitoa
pongezi kwa uongozi wa Mahakama ya wilaya ya Mbarali kwenye kufuatilia suala la
viwanja kwa haraka kama ilivyoelekezwa kuelekea lengo la Mahakama ya Tanzania
kuwa na Mahakama katika kila Kata.
Katika
ziara hiyo, Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu kanda ya Mbeya Mhe. Tiganga
aliambatana na viongozi wengine wa Mahakama akiwemo Naibu Msajili Mfawidhi
Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Aziza Emily Temu, Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe. Zawadi Laizer na Afisa Utumishi Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mbeya Bi. Paulina Kaaya.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) akiwa kwenye
pamoja na watumishi wa Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Songwe.wa kwanza kulia ni
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi. Mavis Francis Miti, wa kwanza
kushoto ni Mtendaji wa Mahakama kuu Masijala ndogo ya Songwe Bw. Sostenes Mayoka,
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akipokea maelezo maalum wakati wa alipokuwa akikagua maendeleo ya
mradi wa ujenzi wa Kituo Chumuishi Songwe.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akikagua maendeleo ya
mradi wa ujenzi wa Kituo Chumuishi Songwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni