Na SOJO STEPEHEN-Mahakama, Mtwara
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki, amefanya ziara ya
ukaguzi wa Mahakama za Mkoa wa Mtwara ili kujionea utendaji kazi, hasa katika
Mahakama za ya chini na kati kuhakikisha huduma ya utoaji haki inaendelea
kufanya vyema.
Ziara hiyo ilifanyika tarehe
23 mpaka 25, Machi 2026. Miongoni mwa Mahakama zilizokaguliwa na ni Mahakama ya
Hakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya Tandahimba, Newala, Nanyumbu, Masasi, Mahakama
za Mwanzo Makuta, Mkunya, Mchaulo na Lukuledi.
Ziara hiyo pia
ilijumuisha mazungumzo ya pamoja na Watumishi wa Mahakama alizopita kwa ajili
ya ukaguzi. Aliweza kupata taarifa za utendaji kazi, mafanikio, changamoto, mapato
na matumiz.
Aidha, Jaji Mfawidhi pia alipokea
mawazo na maoni kutoka kwa Watumishi wa Mahakama hizo na kuhimiza weredi wa
kuihudumia jamii inayowazunguka.
Mhe. Kakolaki aliwapongeza
Mahakimu na Watumishi wa Mahakama kwa utendaji bora na mzuri, hasa kumaliza
mashauri kwa wakati, kutokuwa na mlundikano na kuwa na aina bora ya utunzaji
kumbukumbu.
Katika ukaguzi huo pia, Jaji
Mfawidhi aliwapongeza Watumishi wa Mahakama katika matumizi wa mifumo ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo inawezesha kufuatilia na kusikiliza
mashauri kwa njia ya mtandao. Aliwasisitiza kuendelea kuwaelewesha Wananchi
kwenye matumizi ya mifumo hiyo ili kupunguza gharama za kila mara.
Katika ziara hiyo, Jaji
Mfawidhi aliambatana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe.
Seraphine Nsana, Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Kanda ya Mtwara, Bw. Yusuph
Msawanga na Msaidizi wa Sheria wa Jaji Mfawidhi, Mhe. Stella Shindika
Jaji Mfawidhi pia alitembelea na kukagua Mahakama za Mwanzo zilizokuwa katika ujenzi na zile ambazo zilizokuwa tayari zimekamilika. Aidha, aliendelea kusisitiza ujenzi ufanyike kwa kuzingatia ubora na kwenda kwa wakati.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki akipokelewa na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Newala.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki, (wa tano kulia) katika picha ya pamoja na Watumishi alipotembelea Mahakama ya Mwanzo Mahuta Wilaya ya Tandahimba.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo
Mkunya Wilaya ya Newala Mhe. Apatesile Mbalasila(kushoto), akisoma taarifa fupi
ya Mahakama hiyo mara baada ya kumkaribisha Jaji Mfawidhi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto) akiwa na Mhe. David Msalilwa(katikati), Mhe Charles Mnzava (kulia) katika mazungumzo na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Tandahimba.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki akitembelea Mahakama ya
Mwanzo Mchauru.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki akiwa anakagua jengo la
Mahakama ya Mwanzo Mchauru, ambalo lilipata maafa na kusababisha uharibifu.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki akikagua ujenzi wa jengo
la Mahakama ya Wilaya Masasi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki katika picha ya pamoja na
Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Nanyumbu.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni