Jumapili, 12 Aprili 2026

JAJI MFAWIDHI SONGWE AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Na. Iman Mzumbwe – Mahakama, Songwe

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Songwe imefanya kikao cha Baraza la wafanya kazi kilicholenga kujadili maswala muhimu ya kiutumishi, kuimarisha utendaji kazi na kutunza maadili ya kiutumishi miongoni mwa watumishi.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 10 Aprili, 2026 katika Ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe, ambapo kiliongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Songwe Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songwe Mhe. Gabriel Pascal Malata na kuwakumbusha watumishi kutunza maadili na uwajibikaji kazini na mshikamano mahala pa kazi.

Mhe. Malata alifungua kikao na kusoma ajenda mbalimbali ambazo ziliambatana na uchaguzi wa viongozi waliopendekezwa na wajumbe wa Baraza la wafanya hilo ambapo walipigiwa kura, huku wasimamizi wa uchaguzi huo wakiwa ni Katibu wa Tughe Mkoa wa Songwe Bi. Magreth Emmanuel Mwantebwa na Afisa kazi Mkoa wa Songwe Bi. Pendo Eva Lugendo.

Mhe. Malata alitumia kikao hicho alitoa neno la shukurani kwa viongozi na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Songwe walioshiriki katika kikao hicho huku akisistiza kuendelea kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao mahala pa kazi.

Vilevile, Mhe. Malate aliwahimiza Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), viongozi wa matawi Tughe pamoja na viongozi wa Mahakama kuendelea kuwasisistiza watumishi kujiunga na chama cha Tughe mahala pa kazi kwani chama hicho ni muhimu na ni kwa mujibu wa sharia za vyama kazini. lakini pia ni muhimu kwa sababu ya kutatua changamoto za watumishi na kutetea stahiki za watumishi kwa ujumla.

Aidha, wajumbe wa Baraza hilo walipata fursa ya kuwasilisha hoja na mafanikio waliyoyapata katika kipindi kilichopita, changamoto zinazowakabiri watumishi pamoja na mikakati ya kuboresha mazingira ya kazi.

Sehemu ya changamoto zilizowasilisha ilikuwa pamoja na uhitaji wa mafunzo endelevu kwa watumishi wa Mahakama kwani kumekuwa  na maendeleo ya teknolojia inayohitaji mafunzo ili kuweza kuendana na mifumo mbalimbali ya utendaji kazi kwa watumishi.

Baraza hilo lilisisitiza umuhimu wa kuzingatia miongozo ya utumishi wa umma na sheria zinazosimamia utendaji kazi, wajumbe walihimizwa kudumisha mshikamano na kuheshimiana kazini ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu.

Kikao hicho kilihudhuliwa na wajumbe kutoka Mahakama ya Mkoa Songwe na Mahakama za wilaya kama vile Mbozi, Momba, Ileje, Songwe na Wengine walikuwa ni Katibu wa TUGHE Mkoa Songwe Bi. Magreth Emmanuel Mwantebwa na Afisa kazi Mkoa wa Songwe Bi. Pendo Eva Lugendo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Pascal Malata na Mwenyekiti wa kikao hicho cha Baraza la wafanya kazi (kushoto) akiwa Meza Kuu na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Songwe Bw. Sostenes Mayoka (kulia) wakifuatilia kwa karibu shughuli za Baraza kwenye kikao hicho.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Pascal Malata na Mwenyekiti wa kikao hicho cha Baraza la wafanya kazi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na katibu wa Baraza la wafanya kazi Mhe. Mesia Gang’olo (kulia) na Katibu msaidizi Bi. Joyce Simba (kushoto) ambaye pia ni Msaidizi wa kumbukumbu katika Mahakama ya Wilaya ya Momba - Songwe


Katibu wa Baraza la wafanya kazi Mhe. Mesia Gang’olo (kulia) na Katibu msaidizi Bi. Joyce Simba (kushoto) ambaye pia ni Msaidizi wa kumbukumbu katika Mahakama ya Wilaya ya Momba - Songwe wakiwa wanatabulishwa mara baada ya uchaguzi

Katibu wa TUGHE Mkoa Songwe Bi. Magreth Emmanuel Mwantebwa na Afisa kazi Mkoa wa Songwe Bi. Pendo Eva Lugendo wakihesabu kura zilizopigwa na wajumbe wa Baraza hilo kuwachagua Viongozi.

Sehemu ya wajumbe wa kikao cha Baraza la wafanya kazi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe wakifatila kinachoendelea katika kikao hicho cha Baraza la wafanya kazi.

Jaji Mfawidhi  wa Mahakama Kuu Kanda ya Songwe Mhe. Gabriel Malata (hayupo pichani) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao wakiimba wimbo wa mshikamamo.


Afisa kazi Mkoa Songwe Bi. Pendo Eva Lugendo akikabidhi mkataba kwa Mwenyekiti wa Baraza la wafanya kazi Songwe Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songwe Mhe. Gabriel Malata wakati wa kikao hichokilichofanyika katika katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe.

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni