Na HIGHNESS TERRY-Kituo Jumuishi cha Masuala Familia,Temeke
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Mahakama Kuu Kituo Jumuishi cha Masuala
ya Familia Temeke limefanyika hivi
karibuni kujadili ustawi wa Watumishi,
tathmini ya utekelezaji wa maazimio yaliyopita, pamoja na kupanga mikakati ya
kuboresha utendaji kazi wa Taasisi.
Kikao
hicho kilichofanyika kwenye Ukumbi
wa Mikutano kwenye Kituo hicho kilikuwa jukwaa muhimu la
majadiliano ya wazi kati ya uongozi na Watumishi,
kikilenga kuimarisha uwajibikaji, uwazi na ushirikishwaji katika masuala ya
kiutumishi.
Kikao
hicho kiliongozwa
na Kaimu Jaji Mfawidhi, Mhe.
Sarah Mwaipopo. Katika hotuba yake ya ufunguzi, alisisitiza umuhimu wa Baraza
kama chombo cha kushauri na kuimarisha mahusiano kazini.
Mhe.
Mwaipopo alieleza
kuwa, “Baraza hili ni jukwaa la kujenga Taasisi yetu kwa pamoja,
hivyo mawazo yenu ni msingi wa maboresho
tunayoyahitaji.”
Katika kikao hicho, kulikuwepo pia na ajenda
ya uchaguzi wa Viongozi wapya wa Baraza. Hivyo
aliwashukuru na kuwaaga Viongozi wa Baraza waliopita, Bi.
Fatuma Jumbe,
aliyekuwa Katibu na Bw. David Mbago, aliyekuwa Katibu Msaidizi.
Zoezi
la uchaguzi lilisimamiwa na Ofisa
Kazi, Bw. Hussein Mwamba, ambaye
alisisitiza taratibu za uchaguzi kuwa wazi na shirikishi kwa wajumbe kwa mujibu
wa Mkataba.
Baada ya wajumbe kupiga kura, Bw. David Mbago alichaguliwa kuwa Katibu mpya wa
Baraza, huku Bi. Fatuma Jumbe akawa Katibu Msaidizi. Bi.Doroth Ndunguru alichaguliwa kuwa Mwakilishi TUGHE.
Katika
tathmini ya utekelezaji wa maazimio ya kikao kilichopita, Baraza liliridhishwa
kubaini kuwepo kwa hatua kadhaa chanya zinazoonesha juhudi za uongozi katika
kuboresha ustawi wa Watumishi
na ufanisi wa utendaji kazi.
Pamoja
na mafanikio yaliyopatikana,
Baraza lilibaini kuwepo kwa changamoto kadhaa zinazoendelea kuathiri
utekelezaji wa maazimio na ufanisi wa kazi kwa ujumla. Changamoto hizo
zinahitaji kushughulikiwa kwa umakini ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Watumishi waliibua hoja ya kuchelewa kupandishwa madaraja, hususan kwa wale walio kwenye ajira za muda mrefu. Katika mjadala, ilisisitizwa kuwa Watumishi wanapaswa pia kujitahidi kujiendeleza kielimu ili kukidhi vigezo. Aidha, wajumbe walisisitiza umuhimu wa kutoa elimu kuhusu Miundo ya Utumishi ili kuondoa mkanganyiko.
Baraza linasisitiza umuhimu wa kuendeleza mafanikio yaliyopatikana huku likichukua hatua za haraka na za kimkakati kushughulikia changamoto zilizobainika.
Katikati
ni Kaimu Jaji
Mfawidhi
wa Mahakama
Kuu Kituo
Jumuishi
Temeke, Mhe. Sara Mwaipopo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza
la Wafanyakazi. Kushoto ni aliyekua Katibu wa Baraza, Bi. Fatuma Jumbe na
kulia ni aliyekua
Katibu
Msaidizi, Bw. David Mbago.
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Hamisi Some, akichangia Hoja katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi.
Bw. David Mbago aliyekuwa Katibu Msaidizi akiwashukuru wajumbe kwa nafasi ya kuwatumikia.
Katibu na Katibu Msaidizi wakiwashukuru wajumbe kwa kuwapigia kura za
kuwachagua katika awamu nyingine ya uongozi.
Bwana Hussein Mwamba, mjumbe kutoka Baraza Kuu la Wafanyakazi
katika kusimamia zoezi la uchaguzi wa Katibu, Katibu Msaidizi na Mjumbe
Mwakilishi katika Baraza la
TUGHE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni