Na. MWINGA MPOLI – Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga
ambaye ni Mweneyekiti Baraza la wafanyakazi Mahakama Kuu aliongoza watumishi wa
Kanda hiyo kuendesha baraza hilo katika kujadili mambo mbalimbali yanayohusu watumishi
ili kuendelea kujenga umoja, maadili na mshikamano mahali pa kazi.
Akiongea
katika kikao hicho kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano
Mahakama Kuu Mbeya. Mwenyekiti huyo wa Baraza alisema, umuhimu wa kikao hicho
ni kujadili dira ya taasisi kimkoa, kikanda na kuelezea muelekeo wa utekelezaji
wa majukumu kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
“Nawaomba
wajumbe kuwa wawazi katika kutoa Mawazo ya kujenga taasisi, mkikumbuka kwamba
mnawawakilisha watumishi zaidi ya 300 katika kikao hiki lakini pia mkawe
mabalozi wa kuwasilisha yale yote yaliyojadiliwa hapa,” alisema Mhe. Tiganga,
Kikao
hiki kulihudhuriwa na Maafisa wawili kutoka TUGHE na wajumbe mbalimbali kutoka
Mahakama kwa mujibu wa Mkataba mpya wa Baraza la wafanyakazi wa Mahakama.
Aidha
katika kikao hicho pia kulifanyika uchaguzi wa kuwachagua Viongozi ambao ni
Katibu na Katibu Msaidizi wa Baraza la wafanyakazi wa Mahakama Mkoa wa Mbeya na
uchaguzi wa wajumbe wawakilishi wawili wa baraza kuu Taifa kufuatia wale
waliokuwepo muda wao kuisha.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga
(kushoto) akiongoza kikao hicho cha Baraza na kulia ni Katibu wa Baraza la
wafanyakazi Mahakama Mkoa wa Mbeya Bw. Alintula Ngalile.
Katibu wa Baraza la wafanyakazi Mahakama Mkoa wa Mbeya Bw. Alintula Ngalile akielezea jambo katika kikao hicho.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga (katikati)
kulia ni Afisa kutoka Tughe (aliyesimama) kushoto ni Katibu wa Baraza la
wafanyakazi Mahakama Mkoa wa Mbeya Bw. Alintula Ngalile.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni