Na. CHRISTOPHER MSAGATI–Mahakama, Manyara
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Manyara, Mhe. Ilvin Claud Mugeta,
amewaongoza watumishi wa Mahakama Kanda hiyo, kufanya ziara ya utalii wa ndani
iliyofanyika mnamo tarehe 10, Aprili 2026 katika Hifadhi ya Taifa Tarangire mkoani
Manyara.
Akizungumza
na watumishi kwa nyakati tofauti wakati wa maandalizi na hitimisho la ziara
hiyo, Mhe. Mugeta alieleleza lengo la ziara hiyo ni kutambua maeneo mapya
ambayo watumishi wengi hawajawahi kuyafikia, kupata furaha na kuimarisha afya
ya akili.
“Muda
mrefu tunakaa ofisini tukiwa tunashughulika na majukumu ya usikilizwaji wa
mashauri bila kupata fursa ya kufahamu masuala mengine mengi ambayo tunapaswa
kuyafahamu. Hili jambo linaweza kupunguza ufanisi wa utendaji kazi kama
tunakosa muda wa kuwaza masuala mengine nje ya kazi, ziara hii ya Tarangire
ituwezeshe kuwa na mtazamo mpya lakini pia kuyafahamu maeneo ambayo
yanatuzunguka,” alisema Mhe Mugeta.
Kwa
upande wake, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Manyara Mhe. Devotha Kamuzora
aliwapongeza watumishi wote waliofanikiwa kushiriki ziara hiyo na kuwashauri
watumishi kuendelea kushirikiana katika masuala kama hayo yanapojitokeza kwa
kuwa pia yanaongeza upeo wa ufahamu ambao unaimarisha utendaji kazi.
“Nawapongeza
watumishi wote ambao no watalii wenzangu waliofanikiwa kusafiri kwa ajili ya
utalii wa ndani, nawashauri siku nyingine ziara kama hii ikitokea tuungane sote
kwa pamoja kwa kuwa tutakuwa tumeongeza kitu kikubwa sana katika upeo na
ufahamu wetu na kuboresha ufanisi wa kazi,” alisema Mhe. Jaji Kamuzora.
Katika
hatua nyingine, watumishi ambao walikuwa wamepanda basi walikwama kwenye matope
ambayo yamesababishwa na mvua ambazo zinaendelea kunyesha nchi nzima jambo
liliwafanya watumishi hao kushuka kwenye basi na kuanza kulisukuma. Hata hivyo
walijulishwa na waongoza watalii kuwa hayo ni mambo ya kawaida kutokea katika
mbuga na pia ni sehemu ya masuala ambayo yanafanya ziara ipendeze zaidi.
Watumishi
112 wa kada mbalimbali kutoka Mahakama za ngazi mbalimbali wakiwemo Naibu
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara, Mahakimu Wakazi wafawidhi wa
Wilaya zilizopo katika Kanda ya Manyara, Mahakimu na Mtendaji wa Mahakama Kuu
Kanda ya Manyara walishiriki ziara hiyo ikiwa ni muendelezo wa kutambua vivutio
vya asili vilivyo ndani na nje ya Mkoa wa Manyara pamoja na kuwafanya watumishi
kuendelea kuishi kwa umoja na ushirikiano.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mhe. Ilvin Mugeta (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wa Mahakama Kuu
Kanda ya Manyara wakati wa ziara ya kuona Wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya
Wanyama Tarangire.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Manyara Mhe. Ilvin Mugeta (wa nne kutoka kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na watumishi ambao wameajiriwa siku za hivi
karibuni katika ziara ya kuona Wanyama Tarangire.
Watumishi
wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara wakiwa wanasukuma basi lililokwama kwenye
matope wakati wa Ziara ya kuona Wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Wanyama
Tarangire.
Kundi
la Swala wakiwa wanaonekana wakila majani katika Hifadhi ya Taifa ya Wanyama
Tarangire.
Tembo
akiwa anaonekana akila majani katika Hifadhi ya Taifa ya Wanyama Tarangire.
Jaji
wa Mahakama Kuu, Kanda ya Manyara Mhe. Devotha Kamuzora (aliyesimama) mbele,
akitoa neno kwa watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara kabla ya kuanza
safari ya kuelekea Tarangire.
Watumishi
wa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo
la Mahakama Kuu Manyara wakati wakijiandaa kuelekea Tarangire.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
.jpg)

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni