Marehemu Lukio Ezekiel Mrutu enzi za uhai wake.
TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Bw. Lukio Ezekiel Mrutu aliyekuwa Opereta wa Kompyuta Mkuu aliyekuwa akihudumu Mahakama Kuu Kanda ya Moshi.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Bi. Maria Francis Itala marehemu Lukio amefariki dunia saa 8 usiku wa kuamkia leo tarehe 13 Aprili, 2026 katika Hospitali ya Rabininsia iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Bi. Itala amesema, taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa na mara baada ya
kukamilika taarifa za mazishi zitatolewa.
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unatoa pole kwa
familia, ndugu, jamaa na marafiki na watumishi wote kufuatia msiba huu mkubwa wa kuondokewa na mpendwa wetu.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni