Alhamisi, 2 Aprili 2026

MENEJIMENTI YA MAHAKAMA KANDA YA MUSOMA YAFANYA UTALII SERENGETI

Na KANDANA LUCAS-Mahakama, Musoma

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya, amewaongoza wajumbe wa menejimenti kutembelea mapori ya akiba Ikorongo na Grumeti yaliyopo katika Hifadhi ya Wanyama Serengeti kwa ajili ya kufanya utalii.

Ziara hiyo ilifanyika baada ya kuhitimisha kikao cha menejimenti kilichofanyika mwishoni mwa mwezi Machi 2026. Ziara hiyo pia ililenga kuwapa fursa wajumbe na Watumishi wengine wa Mahakama kupata mapumziko mafupi na kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu uhifadhi wa Wanyamapori.

 Katika ziara hiyo, wajumbe waliweza kutembelea maeneo yenye Wanyama mbalimbali na walipatiwa elimu kuhusu uhifadhi na namna Wahifadhi wanavyokabiliana na changamoto za ujangili.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (mwenye kofia) na Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Musoma, Bw. Leonard Maufi, wakionesha kundi la Wanyamapori (hawapo pichani).

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya akiwaongoza wajumbe wa menejimenti kufanya utalii wa kupanda mlima.

Kundi la Nyati wakiwa kwenye moja ya mapori ya akiba katika hifadhi ya Wanyama Serengeti.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati mwenye kofia mstari wa mbele) akiwa na  Viongozi wa mapori ya akiba Ikorongo na Grumenti pamoja na wajumbe wa menejimenti.

Meneja Mahusiano kutoka Grumeti Fund, Bw. David Mwakipesile, akitoa elimu ya uhifadhi wa Wanyamapori kwa wajumbe wa menejimenti (hawapo pichani).

Picha za wanyama Simba akiwa porini, mmoja akiwa juu ya mti huku mwingine akitembea.

Picha ya wajumbe wakiwa kwenye magari ya watalii.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhe. Monica Ndyekobora, akitoa neno kwa wajumbe wa menejimenti (hawapo pichani) wakati wa ziara ya utalii.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni