Na HIGHNESS TERRY-Kituo Jumuishi cha Masuala Familia,Temeke
Mahakama
Kuu Kituo Jumuishi cha Masuala ya Ndoa na Familia Temeke, hivi karibuni
ilifanya kikao cha menejimenti kujadili mambo mbalimbali ya kiuntendaji.
Kikao
hicho kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano kwenye Kituo hicho kilihusisha
uongozi wa Mahakama pamoja na watumishi wa vitengo mbalimbali kwa lengo la
kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa majukumu, kupima mafanikio,
kuchambua changamoto na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji wa mahakama.
Kaimu
Jaji Mfawidhi, Mhe. Sarah Mwaipopo, aliongoza kikao hicho kusisitiza umuhimu wa
uwajibikaji, ushirikiano na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu ya kila
siku ya utoaji haki.
Katika
kikao hicho, wajumbe walipokea taarifa ya kipindi cha Januari hadi Machi 2026 kutoka
kwa Ofisa Utumishi wa Mahakama, Bi. Jennifer Malisa, aliyekuwa mjumbe wa kikao
hicho.
Alieleza
kuwa Mahakama katika Kituo Jumuishi Temeke imeendelea kufanya kazi kwa ufanisi
katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma kwa wateja wanaofika mahakamani hapo,
hivyo kuelezea mafanikio, changamoto na mikakati iliyofanywa katika kipindi cha
miezi mitatu iliyopita.
Moja
ya mafanikio makubwa ni kuendelea kuboreshwa kwa huduma za usikilizaji wa
mashauri kwa kutumia teknolojia na huduma za Mahakama Inayotembea
zilizoanzishwa katika Wilaya zote kwa Dar es salaam, hali iliyosaidia kupunguza
gharama na muda kwa wahusika walioko mbali na Kituo.
“Mifumo
ni jjambo endelevu na lenye tafsiri
pana, ambapo bado tunaendelea kufanyia kazi katika kubuni ili kurahisisha
ufanisi wa kazi,” aliongeza Bw. Fredrick Kachenje, katika kuelezea mafanikio na
umuhimu wa TEHAMA katika jukumu zima la kutoa haki kwa Watanzania.
Pamoja
na hayo, Mtendaji wa Mahakama Kituo Jumuishi Temeke, Bw. Samsoni Mashalla, alileza
juhudi wanazozifanya katika kupeleka wataalamu wa TEHAMA kupata mafunzo kwa Mahakama
nyingine, ikiwemo matumizi yasiyo na karatasi ili kuchukua ujuzi.
Aidha,
Mahakama imefanikiwa kuimarisha mifumo ya kiutawala na usimamizi wa mashauri
kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wa kila siku. Watumishi wameendelea
kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kujenga uwezo na kuboresha utoaji huduma ndani
nan je ya kituo.
Halikadhalika,
Mtendaji alieleza juu ya mafunzo yanayotolewa kwa wateja nje na na ndani ya
kituo kwa ajili ya kuogeza uelewa juu ya haki zao na upatikanaji wa haki
unaotolewa kituoni hapo.
Katika
upande wa miundombinu, baadhi ya marekebisho ya vitendea kazi na majengo
yamefanyika, pamoja na ukarabati wa vyombo vya usafiri na vifaa vya ofisi, huku
jitihada za kuboresha mazingira ya kazi zikiendelea.
Licha
ya mafanikio yaliyopatikana, kikao kilibaini changamoto mbalimbali zinazoathiri
ufanisi wa utoaji huduma za Mahakama. Changamoto kubwa ni upungufu wa Watumishi
na vitendea kazi, hali inayoathiri mazingira ya kazi na ufanisi wa Watumishi.
Mtendaji
alieleza pia ufinyu wa bajeti ambao umeathiri utekelezaji wa baadhi ya shughuli
muhimu ikiwemo matengenezo ya vifaa, ununuzi wa vitendea kazi na kuboresha
miundombinu ya ofisi.
Changamoto nyingine ni katika usimamizi wa mirathi ambapo baadhi ya mirathi hazifungwi kwa wakati, pamoja na changamoto za usimamizi wa fedha zake katika akaunti ya mirathi iliyoko mahakamani hapo kuendelea kupokea fedha.
Kaimu Jaji Mfawihidhi wa
Mahakama Kuu Kituo
Jumuishi
Temeke, Mhe.
Sara Mwaipopo akiongoza kikao cha menejimenti.
Mtendaji wa Mahakama Kituo Jumuishi Temeke, Bw. Samson Mashalla, aliyekuwa Katibu katika kikao hicho
akifafanua jambo.
Ofisa TEHAMA, Bw. Fredrick
Kachenje,
akifanya wasilisho juu ya mafanikio ya mifumo ya TEHAMA katika kipindi cha robo
ya tatu ya mwaka
katika
kikao
hicho.
Wajumbe wa menejiment
wakisikiliza mawasilisho katika hicho.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni