Na FRANCISCA SWAI – Mahakama, Musoma
Msajili Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya, amewaasa Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala
Ndogo Musoma kuilinda hadhi ya Mahakama kupitia utendaji wao wa kazi na hata
katika maisha nje ya kazi.
Mhe. Nkya alitoa wito huo jana tarehe 29 Aprili, 2026 alipofanya kikao kazi na Watumishi hao
pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma.
Awali akifungua kikao
kazi hicho, Mhe Nkya alisema yuko Musoma kwa siku tatu kwa ajili ya ufuatiliaji
na tathmini ya shughuli mbalimbali za kimahakama ambazo zimefanyika katika baadhi
ya Mahakama za Masjala Ndogo Musoma.
Vilevile kupitia kikao
hicho, Mhe. Nkya aliwasisitiza Watumishi kupenda kujisomea ili kujiongezea
maarifa ya vitu tofauti vitakavyoboresha utendaji wao wa kazi, afya na maisha kwa
ujumla.
Kupitia kikao kazi hicho,
Watumishi mbalimbali walipata nafasi ya kuwasilisha hoja, changamoto na
mapendekezo ya maboresho mbalimbali ili kuboresha mazingira ya kazi, maslahi na
huduma kwa mteja.
Aidha, pamoja na
ufuatiliaji na tathmini ya shughuli mbalimbali za kimahakama Mhe. Nkya
alikabidhi vifaa vya kazi ambavyo ni kompyuta mpakato kwa Majaji wa Mahakama
Kuu Musoma.
Katika ziara hiyo, Msajili Mkuu ametembelea Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, Mahakama ya Wilaya Musoma, Mahakama ya Wilaya Butiama, Mahakama za Mwanzo Musoma Mjini, Mukendo na Kukirango na kote alikopita ameongea na Watumishi wa maeneo hayo.
Msajili Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania, Mhe Eva Nkya (aliyesimama) akiwasalimia watumishi wa Mahakama Kuu
Musoma na Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma wakati wa kikao kazi hicho.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Omary Kingwele (aliyesimama) akimkaribisha Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe Eva Nkya (aliyeketi mbele katikati) wakati wa kikao kazi na Watumishi wa Mahakama Musoma.
Mkurugenzi wa
Ufuatiliaji, Ukaguzi na Mrejesho wa Huduma za Mahakama, Mhe. Maira Kasonde (wa
pili kushoto) akichangia jambo wakati wa kikao kazi na watumishi wa Mahakama
Musoma.
Sehemu ya Viongozi wa
Mahakama Kuu Musoma na Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma wakifuatilia kwa makini
kikao kazi cha Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe Eva Nkya (aliyeketi
mbele katikati) wakati wa kikao kazi na Watumishi wa Mahakama Musoma.
Watumishi wa Mahakama Kuu
Musoma na Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma wakimsikiliza kwa makini Msajili Mkuu
wa Mahakama ya Tanzania, Mhe Eva Nkya (aliyeketi mbele katikati) wakati wa
kikao kazi na Watumishi wa Mahakama Musoma.
Msajili Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania, Mhe Eva Nkya, akizungumza wakati wa kikao kazi na Watumishi wa
Mahakama Musoma.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Musoma, Mhe. Marlin Komba (kushoto) akipokea
kompyuta mpakato kutoka kwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya
(kulia) alipokuwa katika ziara ya Mahakama Musoma.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Geita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni