Na. SHARIFU MOKIWA- Mahakama, Sumbawanga
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga ilifanya Kikao cha Menejimenti tarehe 10
Aprili, 2026 kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji na
kuimarisha utoaji wa huduma za haki kwa wananchi.
Kikao
hicho kilifunguliwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Sumbawanga Mhe, Frederick Manyanda ambaye aliwakaribisha Wajumbe kushiriki
kikamilifu katika majadiliano kwa lengo la kuboresha utendaji wa Mahakama Kanda
hiyo.
Aidha, katika Kikao hicho Mtendaji Mkuu Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Essaba alisoma Muhtasari wa kikao ulifanyika tarehe 2 Aprili 2025 na kupitishwa rasmi na wajumbe ambapo uliidhinishwa kusainiwa.
Hata hivyo Wajumbe walipitia
utekelezaji wa maazimio yatokanayo na Kikao kilichopita ambapo mambo mbalimbali
yalijadiliwa kwa kuzingatia agizo la kikao hicho.
Pia taarifa hiyo ya utekelezaji 2025/2026 iliwasilishwa Mtendaji ikionyesha hali ya raslimali watu, maendeleo ya kiutendaji pamoja na utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
Aidha, baada ya uwasiliswaji wa taarifa hiyo wajumbe walijadili masuala mbalimbali ya kiutendaji kwa lengo la kuboresha utendaji kazi, usimamizi wa raslimali na utoaji huduma kwa wananchi
Kupitia Kikao hicho Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga Mhe. Frederick Manyanda aliunda Kamati ya watu wa watano ambao ni Naibu Msajili, Afisa TEHAMA, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Msaidizi wa Kumbukumbu mmoja na Mwandishi mwendesha ofisi mmoja kwa ajili ya kushughulikia yale maeneo ambayo utekelelezaji wake ni hafifu.
Kwa upande wake, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga Mhe. Thadeo Mwenempazi aliwasisitiza Mahakimu wa Mahakama za Wilaya wanapopokea rufaa kutoka Mahakama za Mwanzo wawe wanaingiza kwenye mfumo wa e-CMS taarifa za majalada yaliyotoka Mahamaka za Mwanzo kama vile mienendo ya mashauri (proceedings), nakala za hukumu pamoja na vielelezo ili kurahisisha utendaji kazi.
Kikao hicho kilihitimishwa kwa wito
kwa wajumbe kuhakikisha utekelezaji wa maamuzi yaliyofikiwa unafanyika kwa
wakati na ufanisi ili kuimarisha utoaji wa haki kwa wananchi.
Sehemu ya wajumbe wa kikao cha
menejimenti wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga
Mjumbe wa kikao
Bw. Mayanga Someke akichangia hoja katika Kikao cha Menejimenti
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni