Jumanne, 14 Aprili 2026

WADAU WAJENGEWA UWEZO KUEPUKA KUTONESHA MAJERAHA KWA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KINGONO

Na FRANCISCA SWAI – Mahakama, Musoma.

Mahakimu, Waendesha Mashtaka na Maofisa Ustawi wa jamii jana tarehe 13 Aprili, 2026 walipatiwa mafunzo ya namna ya kuepuka kutonesha majeraha kwa waathirika wa ukatili wa kingono kabla ya kesi, wakati wa kutoa ushahidi mahakamani na baada ya kesi.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba, akifungua mafunzo hayo yanayotolewa katika ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, alisema mafunzo haya ni mahsusi kwa ajili ajili ya kuwajengea uwezo washiriki katika kushughulikia mashauri ya ukatili wa kijinsia kwa kuzingatia athari mbalimbali wanazopata wahusika, hasa za kiakili na kihisia.

Aidha, Mhe. Komba alisisitiza umuhimu wa washiriki hao kutumia weledi, lugha zenye huruma na staha pamoja na mbinu rafiki katika shughulikia mashauri ya unyanyasaji ili kutowajengea waathirika woga au kumbukumbu mbaya kutokana na majeraha waliyokwisha yapata hapo awali.

Mafunzo hayo ya siku tatu yatagusa maeneo mbalimbali, ikiwemo ushirikiano baina ya Taasisi katika kuwasaidia mashahidi walioko katika mazingira magumu, uelewa wa athari za kiakili na kihisia kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia pamoja na mbinu rafiki na salama za kuuliza maswali ili kuhakikisha utu na hisia za waathirika zinalindwa kuwaondolea woga wanapokuwa wakitoa ushahidi mahakamani.

Washiriki wa mafunzo hayo wametoka Wilaya za Simiyu, Maswa, Meatu, Busega, Sengeti, Tarime, Bunda, Rorya, Bariadi na Itilima.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda yaMusoma, Mhe. Marlin Komba akifungua mafunzo hayo kwa Mahakimu, Waendasha Mashtaka, Maofisa Ustawi wa Jamii yaliyohusu uwezo kuepuka kutonesha majeraha kwa waathirika wa ukatili wa kingono.

Hakimu Mkazi na Mratibu wa mafunzo kutoka Chuo cha uongozi wa Mahakama (IJA), Mhe. Gloria Shuma, akiwakaribisha washiriki wakati wa ufunguzi wa mafunzo haya.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Omary Kingwele (aliyesimama), akitoa neno wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.

Mwezeshaji, Mhe, Venance Mlingi (aliyesimama mbele) akielezea na kusisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zinazoendelea kutolewa na wawezeshaji.

Ofisa Ustawi wa Jamii, Bi. Consolata Makomelo (aliyesimama) akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo.

Muwezeshaji katika mafunzo hayo, Mhe, Nabwike Mbaba (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusiana na atahari za ukatili wa kinsia na kingono.

Wawezeshaji pamoja na washiriki wa mafunzo wakimsikiliza Mwananchi ambaye ndio mara yake ya kwanza kuingia mahakamani, Bi. Elizabeth Roman (aliyesimama kizimbani) aliyeshiriki katika igizo fupi, akielezea uzoefu alioupata kupitia tukio hilo ikiwa ni sehemu ya tathmini ya kujua namna waathirika wa matukio ya ukatili wavyojisikia wakati wa uendeshaji wa mashauri hayo.


Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Marlin Komba (katikati), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Omary Kingwele (kushoto), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Monica Ndyekobora (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo, Mhe. Venance Mlingi (aliyesimama kushoto) na Mhe. Nabwike Mbaba (aliyesimama kulia).

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Marlin Komba (katikati), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Omary Kingwele (kushoto), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Monica Ndyekobora (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote wa mafunzo hayo.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Marlin Komba (katikati), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Omary Kingwele (kushoto), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Monica Ndyekobora (kulia), akiwapamoja na sekretariet ya mafunzo hayo, Mhe. Gloria Shuma (aliyesimama kulia) na Mhe. Prisca Mkeha (aliyesimama kushoto).

Habari hii imeharriwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni