Jumanne, 21 Aprili 2026

WATUMISHI SONGWE WAMUAGA MTUMISHI MSTAAFU

Na. ELIUD KIWANGA – Mahakama, Songwe

Watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe wamemuaga Mtumishi mwenzao Bw. Sigula Simfukwe ambaye alikuwa ni Mlinzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Kishenyi alimpongeza Bw. Sigula Simfukwe kwa kutimiza umri wa kustaafu akiwa na afya njema na alimtakia kila la kheri kwenye maisha yake mapya na pia alimsihi aendelee kuishi kwa upendo na ushirikiano kama alivyokuwa akiishi na Watumishi wenzake mahakamani hapo.

Naye, Mtumishi mwenzake aliyefanya kazi kwa muda mrefu na Bw. Simfukwe mahakamani Bi. Jenitha Sheyo alimpongeza Bw. Simfukwe kwa hatua hiyo na kushukuru kwa ushirikiano wake na kumtakia kila la kheri kwenye maisha yake mapya ya nje ya utumishi wa umma.

Kwa upande wake, Mtoto wa Mstaafu huyo Bw. Joshua Simfukwe alimpongeza baba yake kwa kufikisha umri wa kustaafu akiwa na afya nzuri pia aliwashukuru Watumishi wa Mahakama kwa kumfanyia baba yake hafla hiyo, aliongeza kuwa, hiyo inaonesha baba yake alikuwa akiishi kwa upendo na ushirikiano na Watumishi wenzake mahakamani hapo.

Bw. Sigula Simfukwe aliwashukuru Watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe kwa kumfanyia hafla hiyo ya kumuaga, aliwatakia utumishi mwema watumishi wote wanaobaki mahakamani hapo na kwamba hatasahau nyakati zote nzuri alizopitia mahakamani hapo pia aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano wakati wowote utakapohitajika.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe Mhe. Francis Kishenyi, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbozi Mhe. Nemes Chami na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Mbozi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe, Mhe. Francis Kishenyi (kushoto) na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbozi Nemes Chami (kulia) akifungua hafla ya kumuaga Mtumishi Mstaafu Bw. Sigula Simfukwe.

Mtumishi Mstaafu wa Mahakama Songwe Bw. Sigula Simfukwe akitoa neno katika hafla ya kuagwa kwake.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Mhe. Vitalis Changwe (kushoto) akimkabidhi Bw. Sigula Simfukwe zawadi ya jezi ya Kilabu ya Simba.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbozi Mhe. Nemes Chami (kushoto), akimkabidhi zawadi Bw. Sigula Simfukwe.

Sehemu ya Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Mbozi wakiwa katika hafla ya kumuaga Mtumishi Mstaafu Bw. Sigula Simfukwe.






 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni